SERIKALI YABORESHA MIUNDOMBINU UPIMAJI CORONA

Serikali imefanya maboresho ya miundombinu kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upimaji wa Virusi vya Corona kwa wasafiri wanaoingia nchini.

Hayo yamesemwa leo na katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi wakati alipotembelea uwanja huo akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi(Sekta ya Uchukuzi) Mhe.Gabriel Migire.

Makatibu Wakuu hao wakifika uwanja wa ndege kwa wa ajili ya kujionea maboresho yaliyofanywa kwenye uwanja huo ikiwemo zoezi la upimaji wa Corona kwa wageni wanaoingia nchini. Aidha walitumia muda huo kujionea na kutatua changamoto mbalimbali.

Prof. Makubi amesema kuwa zoezi hilo limeanza muda sasa hapa nchini na kulingana na wasafiri kuongezeka hivyo Serikali imeona ipo haja ya kuboresha miundombinu kila wakati ili kuendana na idadi ya ndege zinazoingia na kuepusha kero za huduma kwa wananchi.

“Suala hili la upimaji sio la sekta moja hivyo tumeona ni vyema kuja pamoja na Katibu Mkuu Mwenzangu na kujionea ili tuweze kuboresha kwa upande wote sote, sasa hivi maboresho makubwa yamefanyika ikiwemo upande wa kutoa majibu ambapo msafiri anapokuwa amelipia anaweza kupata majibu yake moja kwa moja kwenye email yake bila kuchelewa.

Suala la namba ya malipo’control number’ Prof. Makubi amesema kuwa hivi sasa namba za malipo ya upimaji msafiri anaweza kupata hata akiwa nje ya nchi na kulipia hukohuko hivyo kuondoa usumbufu kwa wasafiri,pia wale wanaounganisha ndege wameweza kuwatenganisha kwenye makundi mbalimbali hivyo wanahudumiwa haraka na hivyo kurahisisha zoezi la upimaji. 

Aidha utolewaji wa majibu sasa umekuwa wa muda mfupi na abiria anaweza kutumiwa kwa email , bila kuhitaji kuchapisha cheti.

Aidha, amesema wameweza kuongeza sehemu za upimaji pamoja na watumishi ili kuweza kurahisisha licha ya kuhitaji kuongeza watumishi hao wawe wengi zaidi.

Hata hivyo katibu Mkuu huyo aliwataka wananchi na wageni kujipanga kwa kufuata taratibu za kuachiana hatua moja Kati ya mtu na mtu ili kuweza kuhudumiwa kwa mpangilio na kutokuka

No comments