Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
*https://youtu.be/-P4s8sVq31o*
🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔
.
.
.
Hebu tutazame kuhusu mahari katika biblia je, MUNGU ameruhusu wanaume watoe mahari kwa wazazi wa binti kabla ya ndoa??
Tusome hii
👇👇👇
Mwanzo 2:18,20-25
[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
[20]..................... lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.
[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
[25]Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
.
Ukisoma vizuri kabisa fungu hilo, utagundua kuwa adam hakuomba au hakumwambia MUNGU kuwa """ naomba msaidizi wakufanana naye nitatoa ubavu wangu ili wewe unipatie msaidizi""". BALI MUNGU mwenyewe aliona sio vema adam awepeke yake, angeamua kutengeneza udongo mwingine lakini aliona ni vema achukue ubavu wa adam. Na wala adam hakujua kama MUNGU alikuwa na mpango huo wa kumpatia wa kufanana naye, lakini baada ya kutoka katika usingizi ROHO MTAKATIFU akamfunulia adam yote aliyoyafanya BWANA MUNGU kuhusu kutokea kwa hawa na yeye.
NB
Mstari wa 24 unasema mwanaume atawaacha wazazi wake naye ataambatana na mkewe.
Kwa hiyo wote wanawaacha wazazi wao.
.
Lakini pia ukisoma
👇👇👇👇👇👇
Mwanzo 24:3-4,27,41,48,50-51,53
[3]nami nitakuapisha kwa BWANA, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;
[4]bali enenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke.
[27]Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.
[41]Ndipo utafunguliwa kiapo changu hapo utakapowafikilia jamaa zangu; nao wasipokupa msichana huyo, utafunguliwa kiapo changu.
[48]Nikainama, nikamsujudia BWANA, nikamtukuza BWANA, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, aliyeniongoza njiani, nimtwalie mwana wa bwana wangu binti wa ndugu yake.
[50] *Ndipo Labani na Bethueli wakajibu wakasema, Neno hili limetoka kwa BWANA, wala sisi hatuwezi kukuambia neno jema wala baya.*
[51] *Tazama, huyo Rebeka yuko mbele yako, umchukue, ukaende zako awe mke wa mwana wa bwana wako, kama alivyosema BWANA.*
[53]Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia.
.
.
Utangundua kuwa ibrahimu hakuambiwa atoe mahari kiasi kadhaa bali ibrahimu kwa kuwa alibalikiwa sana kwa mali na fedha na watumwa nk basi aliona vema kuwapa hawa ndugu zake. Lakini sio kama mahari. Kumbuka mstari wa 50,51 hii inaonesha kuwa hawa ndugu baada ya kusikia maelezo ya mtumwa wa ibrahimu wakamruhusu amchukue ndugu yao. Lakini mtumwa akaona ni vema awape fedha na dhahabu nk ambavyo nduguze hawakuviomba au kuvidai.
.
Kwa hiyo ukikubalika kwa wote binti na wazazi. basi wazazi wana bariki kisha unaondoka na binti kuhusu vitu vingine hayo ni maamuzi mengine yako kwa wakristo tu.
.
.
Mahari inaanza kuonekana kwa yakobo alipoenda kuoa kwa mpagani labani ambaye alimwambia ukinitumikia miaka saba basi nakupa binti yangu. kwa hiyo mahari hapa ni kumzalishia kumtunzia vitu vyake.mwanzo 29:18 biblia inaonesha kuwa labani ni mpagani ukisoma mwanzo 31:30,32,34
.
.
.
Lakini kwa wakristo mahari ilitakwa pale tu mtu kampenda binti kisha kamtongoza na akakubaliwa na wakaenda kwa wazazi akakubaliwa kupewa mke kwa hiyo wakawa katika uchumba unao fahamika na kila mtu, sasa mtu mwingine akija, naye akamtongoza binti huyo alieposwa (aliekuwa katika uchumba na mtu mwingine) kwa lugha nyingine kamuiba binti wa mchumba huyo basi aliye muiba atatoa mahari ukisoma Kutoka 22:16,17 au nielezee hivi ili ieleweke mtu akampenda binti kisha wakaenda kwa wazazi, na wazazi wakakubali kuwa ndoa iwepo na ndoa hiyo ikatangazwa, sasa mtu mwingine akaja akamtongoza binti huyo na kulala nae basi lazima atatoa mahali hii ndiyo maana ya fungu hili
Kutoka 22:16-17
[16] *#Mtu #akimshawishi #mwanamwali, #aliyeposwa #na #mume,* #na #kulala #naye, #lazima #atatoa #mahari kwa ajili yake ili awe mkewe.
[17]Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo.
.
😰😰😰😰😰 *MAHARI NI DESTURI YA KIPAGANI* 😰😰😰😰
*biblia inaonesha kuwa mahari ilikuwa ni desturi ya kipagani katika kuoa.* Mwanzo 34:11,12,14,15 imeandikwa """" shekemu akawaambia nikubalike machini penu, na mtakavyo niambia nitatoa, mjapoongeza sana mahari na zawadi nitatoa kadri ya mtakavyo niambia, lakini mnipe huyu msichana
.
.
Kwa fungu hili 👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆 inaonesha wazi kabisa kuwa wapagani kwao sharti *moja* wakukubali *mbili* wakupangie mahari na zawadi kwa ajili ya wazazi na ndugu za binti na wapangaji ni wazazi na ndugu za binti *tatu* wakupe mke.
.
*NB*
SHEKEMU NI MPAGANI UKIPENDA SOMA KISA CHOTE *mwanzo 34*
Lakini kwa watu wa MUNGU haipo hivyo ww ukikubalika tu basi, wanawabariki, wanatangaza uchumba, mwisho unachukua. soma tena mwanzo 24:50,51,52
.
.
.
😂😂😂😂😂😂😂 suala la mahari limewafanya #vijana wengi wasioe kwani vijan wengi hawana pesa wala dhahabu wala majumba hii yote sio kosa lao bali MUNGU ameruhusu hili liwepo maana MUNGU mwenyewe alisema """"" *kwa maana maskini hawata koma katika nchi milele..........* """""" kumbukumbu la torati 15:11 kumbuka pia katika israel yote kulikuwa na watu wa matabaka mbali mbali kulikuwa na matajili na maskini wasomi na wasio soma watumwa na watu huru.
Lakini ni wote walibalikiwa na MUNGU na wote wana uhuru wa kuoa na kuolewa.
*HIVYO MUNGU NDIYE ALIE RUHUSU KUWE NA WATU WA UCHUMI WA JUU, UCHUMI WA KATI NA UCHUMI WA CHINI KWA KILA ANAEMWABUDU. HIVYO TUSIANGALIE KUHUSU MALI BALI TUFURAHI KWA KWENDA KUISHI PAMOJA NAE*
Pia YESU alisema """" kwa maana maskini mnao siku zote pamoja nanyi bali mimi hamnami siku zote""""" yohana 12:8 🤔🤔🤔 je, maskini hawana uhuru wa kuoa au kuolewa kisa hawana mahari?? Kumbuka baraka za MUNGU sio tu kupewa pesa la hasha bali MUNGU anaweza kukubaliki katika afya, maarifa, hekima, busara, nguvu nk.
.
.
.
🏃🏃🏃🏃 😁😁😁 mahari ni upagani ndiyo maana wapagani na wakristo wanao ikubali na kuipokea mahari wanalalamika hasa wale maskini tazama video ya link hiyo apo juu 👆 👆 👆👆👆
.
.
.
Kumbuka utajili unaweza kukutia kiburi cha kujiona ndo umefika na huitaji msaada wowote hivyo unamwasi MUNGU. ndiyo maana YESU alisema """"" ........... Ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajili kuingia katika ufalme wa MUNGU """"" luka 18:25
.
.
👆👆👆
Hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya wenye fedha husingwa na mali zao. Ila masikini mala nyingi hua na ibada.
Tukumbuke kuwa wale ambao MUNGU aliona wanaweza kumtumikia MUNGU wakiwa na mali basi MUNGU aliwapa mali. na wale ambao hawawezi kumtumikia MUNGU na mali basi aliwambia hivi """""" ..........hamwezi kumtumikia MUNGU na mali"""" mathayo 6:24. Kwa hiyo fanya kazi siku sita kwa bidii na maarifa na shauli mbalimbali ukimtanguliza MUNGU mbele lakini siku ya saba sabato (jumamosi) basi pumzika kama BWANA MUNGU alivyo amuru.
lakini pia sherehe za gharama, mapambo ya gharama katika harusi na nguo za gharama. hayo nayo wakristo wameiga tu kwa wapagani na mbaya zaidi kama mahari ikiachwa kutolewa basi masikini wengi hawataweza kumudu hizo ghalama ili wasioe
😱😱 *SIRI NZITO KUHUSU MAHARI* 😱😱
Kwa sababu shetani anajua kuwa BWANA MUNGU karuhusu kuwe na maskini na matajiri. basi shetani kwa kuwatumia wapagani wake, kaingiza mahari na mambo mengi yasiyo na msingi wowote wala umuhimu wowote ambayo yanahitaji fedha nyingi ili watu wasio na uwezo huo wasioe na mwovu huyo akaamua awawashe tamaa wanadam kwa video za ngono na mavazi ya aibu kwa kuwatumia wafuasi wake ili uzinzi na uasherati uongezeke. Dunia igeuke kuwa sodoma na gomola ya zamani. Na walio na fedha wameamshwa tamaa za zinaa ili kuwanunua wadada na akina mama kufanya nao uzinzi na uasherati. Na wa akina mama wengine kwa kutumiwa tu na huyo mwovu wanawanunua vijana ili kufanyanao zinaaa 😭😭😭😭. Hivyo kuendelea kushikilia ulazima wa uwepo wa mahari, sherehe za gharama na mavazi ya gharama ni kuendelea kumsaidia muovu ili uovu uzidi sana.
😂😂😂😂😂 *nilicheka sana kuona video ya link hiyo apo juu kijana akilalamika kuhusu mahari lakini ni kama kweli asemacho* 😂😂😂😂
.
Kama kuna msabato bado anang'ang'ania mahari basi aende akasome """ ( mwongozo wa kanisa la waadventista wasabato ukurasa wa 209, 210).
.
🙏🙏🙏🙏 *tafadhali sambaza kwa wengine* 🙏🙏🙏 kupitia mitandao hapa chini ⏬
Post a Comment