Dalili za kufa Kiroho kwa mkristo
*DALILI ZA KUFA KIROHO KWA MKRISTO NI PAMOJA NA:*
1. Kutoka kwenye familia yako unaenda kwa jirani kupiga soga za umbea, au maseng'enyo juu ya muumini mwenzako au ndoa yako au mtu yeyote yule, alafu ukasahau kuwa agizo ni kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi, wewe unawafanya mataifa kuwa wambea Ole wako!
2. Kwenda kwenye vilabu wewe mkristo kuzungumzia mpira na siasa alafu kwenye suala la kupeleka injilli unasema huwezi kuongea ilihali umbea wa siasa na kuzungumzia mipira unafanya hivyo kwa masaa ya kutosha. Omba Roho Mtakatifu akuhuishe ili hicho kipaji cha kuongea kifanye kazi Yake[MUNGU] na kwa utukufu wake. Kumbuka Mungu hadhihakiwi kamwe.
a) Mzazi kununulia watoto midori ya baiskeli, gari, simu, gemu, kwa bei kubwa lakini hajawa tayari kuwanunulia lesoni, vitabu vya visa vya Biblia(Bible story books) vyenye gharama ndogo. Wazazi wakifa Kiroho watoto ndiyo kabisa kwa sababu Wazazi ndiyo walimu na wachungaji wa watoto wao hawa wakifeli na familia imefeli haswa.
3. Vijana wamekariri miziki ya kidunia yote lakini hata nyimbo za Kristo tano tu hazipo kichwani, basi hata amri za Mungu tu zile Kumi anababaika kuzitaja. Kama haitoshi anaweza kusimlia mkanda wa Muvi aliyoitazama kwa masaa matano kwa marafiki zake pasipo kumsema Yesu hata kwa dakika tano, nani yuko tayari kusimama leo kama Yusufu, au Vijana wale watatu leo? Wanahitajika vijana wenye Roho wa Mungu leo.
4. Shetani kuwaaminisha Vijana kuwa kuoa au kuolewa na mtu asiyeamini ni jambo la kawaida kwamba atamwongoa na badaye akimleta kanisani amwoe au kuolewa naye na hapa ndipo washirikina huongezeka kanisani badala ya kuongeza wafuasi na wnafunzi wa Yesu Kristo. SIMAMA KATIKA NENO NA SI KATIKA TAMAA ZAKO.
5. Kuwa na kifurushi cha meseji 1000 lakini hujawahi kutuma jumbe za matumaini kwa watu ulionao kwenye simu yako hata kuwatakia Sabato Njema tu. Ni Dalili za anguko la Kiroho, meseji zote zinatumika kwa ajili ya tamaa zetu tu.
*Usipokubali kutumiwa na Mungu, Shetani atakutumia vilivyo.*
6. Kukataa na kukana uwepo wa Roho Mtakatifu na kusema hayupo ilihali ukitaka kutenda dhambi ndiye anazungumza ndani ya moyo akikusihi uache kutenda hivyo, mtu wa nmna hii hajafa kiroho tu bali ni Mwasi kabisa. Kumkataa Roho mtakatifu ni kukataa karama za Roho na Huduma yake.
7. Kupuuzia mikusanyiko ya Ibada na maombi; ukisema kuwa Mungu anaangalia moyoni na si nje! Kumbuka Imani bila Matendo imekufa.
8. Kutenda dhambi za siri ili usionwe na viongozi wako wa kanisa kwa kulinda jina la ushirika kwenye kitabu cha kanisa ilihali mbinguni umekataliwa, huu nao ni UBATILI MTUPU.
9. Kubeba chuki ndani ya moyo wako bila kutoa msamaha na bado unasema unamwamini Yesu, NI KUJILISHA UPEPO NA THAMANI YA MSALABA HAIJAFANYA KAZI NDANI YAKO.
10. Kufananisha maisha yako ya Ukristo na muumini mwenzako na kusahau kuwa yeye naye ni mdhambi anahitaji Neema ya Kristo imwokoe. Kielelezo cha maisha na mwenendo wa Mkristo ni KRISTO mwenyewe na si vinginevyo.
*Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;*
2 Timotheo 4:3
*nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.*
2 Timotheo 4:4
SASA TAFAKARI NI WAPI ULIPOANGUKA UKATUBU YESU ANAKUNGOJA LEO.
TUWE NA TAFAKARI NJEMA.
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment