kusuka na unyoaji katika Biblia

KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA.
BWANA YESU asifiwe!😅
Maranatha!😅🙏🏻
Nawakaribisha tena katika somo hili zuri la kuyachunguza maandiko matakatifu kutoka kinywani mwa BWANA MUNGU Muumbaji .
Wapendwa! Kama tukichagua kufa milele, tumechagua sisi wenyewe, hakuna jambo ambalo BWANA ametuficha kuhusiana na maonyo ndani ya kanisa. Yote Huyu Mzee wa SIKU ametuwekea wazi ili tuokolewe. Ila wengi wa Waadventista wasabato wataangamia sababu ya ukaidi wao, na hakika wataangamia.
Swala la kusuka nywele kwa wanawake na mabinti kanisani, Ni MUNGU alikataza kupitia Roho wake mwema kwa kinywa cha petro na paulo mitume wa YESU . Lakini leo watu wamedhani hilo katazo ni fundisho la paulo au petro. Watu wamekuwa na tafsiri za uongo uongo huko makanisani kwamba paulo alikuwa akiwakataza wanawake wa korintho tu, Je Mtume petro alikuwa akiwakataza wanawake wa wapi???
Hii ni dhambi mbaya sana ya kuyashakia maneno ya MUNGU ambayo ni kwaajili ya wokovu wetu. Na kwasababu hakuna wakemeaji ndani ya kanisa kuhusiana na jambo hili la kusuka nywele, kuvaa mawigi, marasta, rangi za midomo na kucha, na nyusi za bandia , na wanja, Ndiyo sababu leo katika makanisa ya Waadventista wasabato duniani kote wanafanana na watu wa mataifa, hakuna utofauti na wapagani. Yani dhambi inayokemewa ni uzinzi tu na ndiyo waumini wanajuwa kuwa iyo ndiyo dhambi🤔. Ingia makanisani siku ya ibada ya sabato, tembeza macho yako kila kona utaona haya niyasemayo.
1Tim 2:9👇🏻👇🏻
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi, si kwa #KUSUKANYWELE wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa ngua za thamani, bali kwa matendo mema...............
Mimi naamini neno la MUNGU wangu halijakisea kabisa, WASABATO HAWASUKI NYWELE, ILA WAPAGANI NDO HUFANYA HIVYO.
Ila kwasababu watu waovu wasiopenda kumsikiliza BWANA wamekuwa wakiwapotosha hawa watu, na hawa watu wamekuwa wakiyaamini maneno ya Wanadamu , baasi wataangamia kama mavi yao wenyewe, Hakika! MUNGU hatanii, hilo lieleweke. Kusuka ni dhambi kwa MUNGU kama zilivyo dhambi zote. Wewe ni binti wa mfalme na Mfalme BWANA hataki usuke nywele zako, je unajuwa ni kwanini amekataa usizisuke???
1Petro 3:3-4👇🏻👇🏻👇🏻
Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, Yaani kusuka nywele, na kujitia dhahabu na kuvalia mavazi. Bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika, yani roho ya upole na utulivu...........
👉🏻 waendee wale wanaosuka, waambie haya maneno, ni wakali na wanarusha mate kama nyoka. Bwana ametutofautisha na walimwengu. Ukiwaambia watakariri mapambio ya wapagani" Mungu haangalii nje bali huangalia moyo" Nani alikudanganya kuwa MUNGU haangalii nje???
Ulivyokatazwa kusuka nywele ndivyo ulivyokatazwa kuvaa mavazi ya wanaume. Waangalie WANAWAKE wanaojinasibu eti ni Waadventista wasabato, nao wanamiliki mavazi ya kiume, suruali. Hivi huu si ni uasi mkubwa?? Wapo mabinti na mama zao huvaa suruali katikati ya juma la wiki, siku ya sabato huyavua na kuvalia vizuri wakidhani MUNGU hakuwaona, ni hivi, BWANA aliwaona na malaika waliwaona, dhambi yenu ipo wazi mbele za MUNGU . Kuvaa suruali mwanamke ni dhambi. Unajifananisha na mwanaume wakati huna maumbile ya kiume, unautaka uanaume wakati siyo stahili yako wewe mama na dada. Unamdhalilisha MUNGU aliyekuumba. Unamchukiza MUNGU wako. Wachukizao hawataingia MBINGUNI kwa BABA.
Kumbukumbu la Torati 22:5👇🏻👇🏻
Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanaume.
👆🏻👆🏻👆🏻hivi ndivyo asemavyo BWANA.
Ufunuo 22:8👇🏻👇🏻👇🏻
Bali waoga na wasioamini, na WACHUKIZAO .......................sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
👉🏻Nyie akina dada na mama , mbona mnataka kufa mara mbili??? 🤔. Ikiwa hamtatubu na kuacha na mkafia dhambini , kufa mara mbili kutawahusu. WAADVENTISTA mmetengwa na walimwengu huu, onyesheni Ukristo sahihi mbele ya jamii inayowazunguka, ili YESU apewe sifa na siyo kusimangwa kila siku.
Vivyo hivyo na wanaume, MUNGU amewakataza kunyoa DENGE, PANKI, KIDUKU, KUCHONGA PEMBE ZA NDEVU ZENU nk, hayo ni machukizo na ni ibada za sanamu. Kichwa cha nyumba uliye mfano wa Kristo, unanyoa denge🤔, unanyoa kiduku🤔, unanyoa hiyo panki🤔, unachonga nywele🤔, unachonga ndevu🤔, Hii balaa. Yani tumepotoka mbele za BWANA na huu ni uasi mkubwa, dhambi hii inatutafuna wanaume. Ingia katika makanisa siku za ibada, angaza macho yako uone vichwa vya wanaume walivyonyoa mitindo ya ibada za kishetani za huko ugiriki, utashangaa. Wengine ni waimbaji wa kwaya, lakini wana denge, panki, kiduku, wamechonga ndevu na pembe za vichwa vyao, huwa nashangaa sana, hivi siku hizi usabato tumeushusha hivi hadi tunafanana na walimwengu??? Makanisani wamejaa wanyoa style za mizimu.
Eti unaambiwa katika kizazi hiki kuna staili ya kunyoa ya kisabato🤔, ninyoe kisabato! We alikwambia nani wasabato tunanyoa Afro! Imeandikwa wapi hiyo Afro! Huo ni umizimu tu.
Mambo ya walawi 19:27👇🏻👇🏻
Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
BWANA amekataza. WAKRISTO wa kweli wataacha, ila bandia hawataacha. Tahiriweni mioyo, asema BWANA .
Yeremia 9:26👇🏻👇🏻👇🏻
Misri, na Yuda, na edomu, na wana wa Amoni, na moabu, na wote wenye KUNYOA DENGE, wakaao nyikani, maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya israeli hawakutahiriwa mioyo yao.🤔
Waisraeli wa leo ni Wasabato , tumekuwa wakaidi mno. Tuache kumpuuza BWANA , la sivyo tujiandae kwa machinjo makuu.
Hata wanaosimamia kazi ya BWANA hawaruhusiwi kunyoa denge vichwani mwao.
Mambo ya walawi 21:1-6.
WACHUNGAJI someni 👆🏻👆🏻👆🏻.
Rafiki mpendwa, kunyoa denge, kuchonga pembe za ndevu, kusuka, kuvaa vitu bandia, yote hayo ni machukizo kwa BWANA wetu. MUNGU anatupenda sana na hapendi tufanye hivyo, tunamuhuzunisha BABA Yetu MTAKATIFU ALIYE JUU.
HEbu fikiria, YESU anakuja ghafla, anakukuta una denge kichwani, umechonga ndevu, una kiduku, umesuka, umevaa suruali ya mwanaume wakati wewe ni mwanamke, na wewe mwanaume umevaa nguo za wanawake, umevaa mawigi, marasta, rangi mdomoni nk nk, hebu fikiria tu, hivi unaweza kumwambia YESU nichukue Juu Mbinguni ??? MBINGUNI ni patakatifu, na wanaoishi pale ni wale waliotii kila andiko la MUNGU .
Tufanye matengenezo. Maisha ni mafupi mno.
YESU anakuja
Na hatakawia
Na ninyi mnaowataharakisha watu katika maandiko! Acheni. Acheni. Acheni neno la MUNGU liseme.
BWANA awabariki.🙏🏻
Share ujumbe huu kupitia Mitandao hapa chini ⏬
Amen mtumishi
ReplyDeleteBarikiwa
DeleteAmen
ReplyDeleteSomo nzuri,sema kuacha ni kazi,Tusaidie na njia za kuacha kusuka
ReplyDeleteAnza kwa kujikana,omba kwa Mungu,anza kuacha taratibu,inawezekana!ondoa hofu!Amen
DeleteNikieka Dawa au kupaka mafuta kwenye nywele Ni dhambi,??
DeleteUbarikiwe
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteAmeni
ReplyDeleteMtumishi barikiwa sana...tunaomba usaidizi jinsi gani tutaweza kuyaacha haya
ReplyDeleteJe kuchonga nywele pia ni dhambi
ReplyDeleteAmina
ReplyDelete