MSHINDI WA BSS KUPATIKANA JANUARY 29
Mshindi wa Shindano la kusaka vipaji, nchini, Bongo Star Search (BSS) anatarajia kupatikana usiku wa Januari 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kiasi cha Sh milioni 20.
Shindano hilo litakalopambwa na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wakiongozwa na, The African Princess @officialnandy, Shishi Baby @officialshilole na mmoja wa majaji wa shindano hilo, Christan Bella @bellachristian1 maarufu kama Mzee wa Masauti.
Akizungumza na vyombo vya habari juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Benchmark na Muandaaji wa Shindano hilo, @msritapaulsen, ‘Madam Rita’ amesema kuwa mwaka huu shindano hilo litakuwa la kitofauti kuanzia washiriki hadi majaji.
“Tunamshukuru Mungu mwaka huu zawadi zitatolewa mapema, mshindi wa kwanza atapata kiasi cha Sh milioni 20, mshindi wa pili atapata kiasi Sh milioni tatu na wa tatu atapata Sh milioni moja,” amesema Madam Rita.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa, (BASATA) Augustino Makame amesema kuwa Waandaaji wameshakabizi zaw
wameshakabizi zawadi za washiriki na sasa wanasubiri mshindi na kumwekea kwenye akaunti yake.
Aidha, ameongeza kila mtu ni mshindi na washiriki watakaoshindana ni wanne na wengine wawili wamepata bahati ya kuchaguliwa na mashabiki hivyo watakuwa jumla ya washiriki ni sita.
#BinagoUPDATES
Post a Comment