AMKA NA BWANA LEO 30/12/2021

Alhamisi 30/12/2021

*TEMBEA KATIKA NYAYO ZA YESU*

*Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake.* *Mathayo 25:15*

Soma maagizo yanayopatikana katika Mathayo 25:14-46. Linganisha maagizo haya na rekodi ya maisha yako. Hebu kila mtu aache kujisifu. Hebu na tutembee katika nyayo za Kristo katika unyenyekevu wa imani ya kweli. *Hebu na tutupilie mbali kujiamini kwote, tukijisalimisha wenyewe, siku kwa siku na saa kwa saa, kwa Mwokozi, tukiendelea kupokea na kutoa neema Yake. Ninawasihi wale wanaokiri kumwamini Kristo watembee kwa unyenyekevu mbele za Mungu*. 

Kujivuna na kujisifu ni chukizo Kwake. *"Mtu yeyote akitaka kunifuata," anatangaza Kristo, "na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate" (Mathayo 16:24).* Wale tu ambao hulitii neno hili Anawatambua kama waaminifu Wake. *"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya watu, bali kwa Mungu" (Yohana 1:12, 13)*.

*"Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu" (Fungu la 14). Unyenyekevu wa pekee jinsi gani! Mfalme wa mbinguni, Kamanda wa majeshi ya mbinguni, alishuka chini kutoka katika nafasi Yake ya juu sana, alilivua vazi lake na taji yake ya kifalme, na kuuvisha Uungu wake kwa ubinadamu, ili aweze kuwa Mwalimu wa kiroho kwa watu wa madaraja yote*, na kuishi mbele za wanadamu maisha huru pasipokuwa na ubinafsi na dhambi, akiwawekea mfano ambao, kwa kupitia neema Yake, wanaweza kuwa.

*"Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, (nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba,) amejaa neema na kweli" (Fungu la 14)*. Mungu atukuzwe kwa kauli hii ya pekee. Uwezekano inaouwakilisha unaonekana kama mkubwa sana kwetu sisi kuuelewa, na kuuaibisha udhaifu wetu na kutokuamini kwetu. 

 *Ninamtukuza Mungu kwa kuwa ninaweza kumwona Mwokozi wangu kwa imani. Roho yangu inaifahamu zawadi hii. Tumaini letu pekee katika maisha haya ni kuufikia mkono wa imani, na kuushikilia mkono ulionyooshwa ili kuokoa. "Tazama Mwana-kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu" (Fungu la 29). Kama tungemtazama Yesu mbali na ubinafsi wetu, tukimfanya kuwa Kiongozi Wetu, ulimwengu utaona katika makanisa yetu nguvu ambayo hauioni sasa.*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*

No comments