SERIKALI YATOA MILIONI 428 KUJENGA DARAJA LA LWELENGULA
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kupitia wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) imetoa kiasi shilingi mil. 428, kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Iwelengula lililopo Manispaa ya Shinyanga mkoani humo, shabaha ikiwa kumaliza kero ya muda mrefu ya ubovu wa daraja husika linalotegemewa na wananchi kata za Kitengula.
Haya yanajiri wakati wa mpango mkakati uliowekwa na Serikali juu ya ukaguzi na ufatiliaji wa Barabara za Mijini na vijijini, ikiwepo ujenzi na ukaguzi wa madaraja ambayo Serikali imejizatiti kuyaimarisha.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa daraja la Iwelengula, wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. David Silinde, amesema, pamoja na ukarabati unaoaendelea katika daraja hilo, Serikali pia imewatuma wahandisi wake kutoka TARURA Makao Makuu, kwaajili ya ukaguzi wa madaraja yaliyoharibika ili yaweze kurekebishwa na kujengwa upya na kuwawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali za kijamii ambazo walikuwa wanashindwa kuzifikia kutokana na mawasiliano kukatika au kutokupitika vizuri hasa nyakati za mvua.
Awali wananchi wa mtaa wa Iwelengula, walimuelezea Naibu Waziri adha wanayowakumbananayo kutokana na kukatika mara kwa mara kwa mawasiliano, hususani kipindi cha mvua, ambapo hali hiyo mbali na kuwasababishia usumbufu lakini vile vile iliendelea kuwakwamisha katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini, ameishukuru Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia TARURA kwakutoa kiasi cha shilingi milioni 428 za kulijenga daraja hilo kwa haraka.
“Mhe. Naibu Waziri, mimi kwa niaba ya wananchi wa jimbo hili, niishukuru Serikali kwa kusikia kilio chetu, kwani wakati wa Bunge la Bajeti nililazimika kutoka bungeni na kwenye vikao vya kamati, kurudi jimboni kwaajili yakusaidiana na wananchi ambao walikua wanateseka kupata huduma za kijamii hasa za afya, kwani daraja hili ndilo linaunganisha wananchi wa kata mbili tofauti ambao wanategemeana katika huduma mbalimbali za kijamii”

Post a Comment