unabii sehemu ya 4,Siku za mwisho zimefika
UNABII WA DANIEL 7:sehemu ya Nne.
Danieli 7:7
👉🏻Badaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama mnyama wa nne , mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma makubwa sana, alikula na kuvunja vipandevipande, na kukanyaga mabaki kwa miguu yake, na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
👉🏻Ufalme huu ulikuwa katili sana
👉🏻Mnyama huyu anawakilisha romapagani/rumi
👉🏻Ni sawa na miguu ya chuma ya sanamu ya nebukadreza. Danieli 2:33,40
👉🏻Ufalme huu ulitawala dunia nzima kuanzia mwaka 168bc hadi 476AD. Luka 2:1-3
👉🏻Pembe kumi ni falme kumi ambazo zilitokea baada ya roma ya kipagani kugawanyika.
TABIA YA ROMA PAGANI
...............................................................
Moyoni mwa warumi hakukuwa na huruma.
Waliangamiza na kuteketeza kabisa miji iliyokuwa ikiipinga roma.
Damu za wapinzani wao zilitapakaa kila mahali.
Warumi walikuwa katili sana, waliwaua adui zao kwa stahili zote za vifo vya uchungu. Dunia yote ya wakati huo ilitiishwa chini ya utawala huu wa romapagani.
JINSI DOLA HII YA ROMA PAGANI ILIVYOGAWANYIKA
.............................................................
👉🏻Makabila makali sana yalishuka kutoka kaskazini mwa ulaya na kuushambulia utawala huu wa romapagani eneo la ulaya magharibi, na kuligawa sehemu kumi. Sehemu hizo ni sawa na vidole kumi vya sanamu ya nebukadreza.
👉🏻wasomi wa historia ya dunia hii wanajuwa vizuri jambo hili ambalo lilitokea mwaka 476AD huko ulaya magharibi.
Makabila hayo ambayo leo ni mataifa yenye uwezo na nguvu za kiuchumi ni👇🏻👇🏻👇🏻
1. Waanglo-saxoni(waingereza)
2. Waalemani(wajerumani)
3. Waheruli(heruli)✓
4. Waostrogothi(ostrogothis)✓
5. Wavandali(vandals)✓
6. Wavisigothi(wahispania)
7. Wasuevi(wareno)
8. Walombadi(waitalia)
9. Waswisi(Switzerland )
10. Wafranks(wafaransa)
Makabila saba kati ya kumi yapo hadi leo yakiwa yamekuwa na kuwa Mataifa ya siku hizi . Mataifa hayo yapo katika ramani ya dunia na ramani ya ulaya kama mataifa yenye nguvu katika karne hii ya 21.
👉🏻Mataifa matatu kati ya yale kumi yalitoweka kabisa katika jukwaa la historia na hayapo duniani leo. Mataifa hayo ni👇🏻👇🏻
Waheruli
Waostrogothi
Wavandali
PEMBE 10 NA PEMBE NDOGO
.......................................................
Danieli 7:19
👉🏻Kisha nalitaka kujuwa maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma na makucha yake ya shaba, aliyekula na kuvunja vipandevipande na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake.
👉🏻mnyama wa nne huyu ni roma pagani/rumi na utawala huu ulianza mwaka 168BC hadi 476AD
(a) Pembe 10
Danieli 7:20
👉🏻na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake.
Pembe 10 ni nini?
Danieli 7:24👇🏻👇🏻
👉🏻 Na habari za zile pembe kumi , katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi
Hivyo, 👇🏻👇🏻
Pembe ni WAFALME
PEMBE 10 NI = na Wafalme 10
👉🏻Kwahiyo pembe 10 zinawakilisha Falme 10 za ulaya magharibi. Falme hizi ni👇🏻👇🏻👇🏻
Uingereza
Ufaransa
Ujerumani
Switzerland
Ureno
Hispania
Waheruli
Wavandals
Waostrogothi
Italia
Naamini mpendwa msomaji hadi hapo umeelewa huu unabii kwa namna ya pekee sana. Unabii ni ramani yetu aliyotupatia MUNGU ili kuzijuwa nyakati tunazoishi na pia kuuona ule mwisho unavyokaribia.
Sasa jiandae kufatilia unabii sehemu ya Tano unaohusu Pembe ndogo iliyozuka katika zile pembe kumi.
Huyu pembe ndogo ni nani?? Fuatana nami mjoli mwenzako , rafiki yako , Pambano Ibrahim Chindema .
Upatapo masomo haya, fundisha na wengine.
BWANA awabariki
Share ujumbe huu kupitia Mitandao hapa chini ⏬
AMEN 🙏
ReplyDelete