BINAGO TUNATOA POLE KUFUATIA JANGA LA MOTO KARIAKOO
#Reposted From MAJIZZO
Nitafutieni mswahili mmoja ambaye biashara yake imeungua kule Kariakoo, anisikilize :
Mwezi Novemba mwaka 2009, Mimi na wafanya kazi Wenzangu Tuliwekeza Nguvu,Akili,Mali na kila kitu chetu pale MaishaClub. Tuliweka Technology ya juu sana yenye gharama kubwa sana ili tuendane na kasi. Niamini hiyo hela tuliichanga zaidi ya miaka 4.Tulifanya matengenezo ya nguvu sana, kila aliyefika pale alikubali kwamba sasa hii ni club ya viwango vya juu.
Siku moja saa 8 mchana, nakutana na moto mkubwa. PAKAUNGUA. Pesa yote, vifaa vyote na kila kitu, viliteketea. Sitaki hata kusimulia sana. Nitakuwa muongo kusema sikuumia, Yes, niliumia sana. Lakini nilisema huu moto hauwezi kuondoka na ndoto zangu, mimi na wenzangu tulijipanga upya kwa nguvu na nia zaidi.
Sikiliza ndugu yangu wa Kariakoo na sehemu nyingine. Najua inauma kiasi gani, nilipitia. Shukuru Mungu kakuachia nguvu zako na akili zako. Ule moto haujaondoka na ndoto zako, kuwa kama kinyonga ambaye akiona moto mwendo wake unaongezeka, kuwa kama dhahabu ambayo ikichomwa inaimarika. Namuomba Mungu akupe nguvu na ujasiri, hili liwe chachu ya kupambana zaidi : #ItakaaSawa

Post a Comment