MHE. MIGIRE ABAINI CHANGAMOTO UWANJA WA NDEGE WA NYERERE

Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi na Uchukuzi (Sektaya Uchukuzi) Mhe. Gabriel Migire amesema ziara walioifanya Kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wameweza kubaini changamoto za vifaa, wataalam na huduma za kibenki ambapo wataalum wa uwanja huo wamewathibitishia kuzishughulikia na kuzipatia ufumbuzi.

Mhe.Migire amesema kuanzia siku ya jumanne wataanza kufuatilia kuona kama changamoto zilizopo kwenye uwanja huo zimepata ufumbuzi ili kama kuna jambo la kufanya jitihada wao watalifanya kazi na kuagiza kuanza kupatia taarifa za vikao vya kila siku kutoka kwa wataalam hao.

Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi Mhe Mingire ameahidi Wizara yake kuendelea kuwa karibu na Wizara ya Afya ili kutatua kwa pamoja changamoto zilizobaki katika viwanja na kuelekeza ifanyike tathimini tena kabla ya Jumanne ya kukabili ongezeko zaidi ya wasafiri/Watalii kwa siku za usoni

Makatibu Wakuu hao wawili, wamewashukuru wafanyakazi wote wanaojituma katika viwanja na mipaka yote na Serikali iko pamoja nao katika kuboresha huduma hizo na kuwaelekeza waongeze usimamizi na uratibu wa pamoja ili kupunguza kero zaidi kutoka kwa wasafiri.

No comments