TITUS AACHILIA ZAIDI YA WAFUNGWA 13 HUKU AKIWA AMELEWA
Afisa wa Polisi Nchini Zambia, Titus Phiri, amekamatwa kwa madai ya kuwaachia huru Wafungwa zaidi ya kumi na tatu ili kusherehekea usiku wa Mwaka Mpya haliyakuwa amelewa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi la Zambia Phiri ambaye ni Mpelelezi wa ngazi ya Inspekta, ametuhumiwa kuchukua funguo za seli kwa nguvu akiwa katika hali ya ulevi kisha kufungua seli za Wanaume na Wanawake na kuwaambia Watuhumiwa kuwa wako huru kuingia mwaka mpya.
Mpaka sasa msako mkali unaendelea kuwatafuta Wafungwa 13 waliotoroka, miongoni mwao wakiwa ni wale wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya unyang’anyi na shambulio.
Aidha Jeshi la Polisi la Zambia limeeleza kuwa litaendelea kushikamana na maadili ya sheria na kuhakikisha kuwa hatua kali zinachukuliwa dhidi ya Maafisa wa Polisi watakaobainika kutumia vibaya mamlaka yao au kwenda kinyume na sheria.
Kwa matangazo wasiliana nasi kupitia 0629567302
Post a Comment