Afisa Gereza mrembo afungwa kwa kufanya mapenzi na mfungwa
Afisa wa zamani wa gereza la HMP Wandsworth ambaye alionekana kwenye video akifanya mapenzi na mfungwa, amepewa hukumu ya miezi 15 jela.
Linda De Sousa Abreu alikamatwa na maafisa wa gereza baada ya video hiyo kusambazwa mtandaoni na kutamba haraka.
Gavana wa gereza la Wandsworth alisema kitendo cha Abreu kilichukua “siku moja” tu kubomoa miaka mingi ya juhudi za kuendeleza mazingira bora kwa wafanyakazi wa kike katika magereza ya kiume.
Abreu, mwenye umri wa miaka 30, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow kabla ya kujaribu kuabiri ndege kuelekea Madrid akiwa na baba yake.
Abreu na mfungwa huyo walionekana kwenye video wakifanya mapenzi katika seli kati ya tarehe 26 na 28 mwezi Juni.
Polisi wa Metropolitan walieleza kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu wafungwa wawili waliotambulika kwenye video hiyo.
Mahakama pia ilielezwa kwamba kuna video nyingine iliyoonekana kwenye kamera aliyovaa Abreu akiwa katika huduma ya gereza, ikionyesha akifanya kitendo cha ngono na mfungwa huyo.
Jaji Martin Edmunds KC alisema video hiyo iliyosambaa mtandaoni siyo tukio moja tu, bali ni sehemu ya tabia ya kurudia.
Chama cha Wafanyakazi wa Magereza, kinachowakilisha wafanyakazi wa gereza, kilikubali kuwa kuna idadi ndogo ya wafanyakazi wapotovu wanaoharibu kazi ya wengine.
Post a Comment