ANTONY MTAKA APIGA MARUFUKU ABIRIA KUSIMAMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameagiza Daladala zote kupakia abiria kulingana na idadi ya viti vilivyoko na kuanzia sasa hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama.

Mtaka ameagiza pia wafanyabiashara katika maeneo yote ya masokoni na kwenye misongamano kuvaa barakoa pia kuwa na maji tiririka na sabuni au vitakasa mikono.

Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo ameagiza kumbi zote za umma na binafsi zinazotumika kufanyia mikutano kuwa na utaratibu wa kugawa barakoa na kutenga sehemu kwa ajili ya kunawa kwa maji safi tiririka na sabuni.

No comments