OUT of the PITCH

Na Kiepo Benedicto

Hebu tufikirie kwa pamoja. 

Aly Ahly klabu kubwa Afrika kwa miaka kadhaa ya karibuni iko chini ya kocha Mwafrika Pitso Mosimane, na amewaongoza kucheza fainali tatu za klabu bingwa Afrika na kutwaa fainali mbili. 

Florent Ibenge ni Mwafrika mwingine huyu raia wa Congo, mwaka wake wa kwanza ameisaidia RS Berkane kutwaa kikombe cha shirikisho barani Afrika. 

Wydad Casablanca ni mabingwa hawa wa kombe la klabu bingwa Afrika. Yule jamaa aliyewaongoza kutwaa kikombe kile, Walid Regragui ni Mwafrika pia. 

Mandla Ncikazi alipewa dhamana ya kuiongoza Orlando Pirates, hakufanya makosa ameifikisha salama fainali ya kombe la shirikisho bahati haikuwa yake, usisahau ni Mwafrika huyu. 

Kuna kitu nimekiona, mpira wa Afrika hivi sasa umetawaliwa na waafrika wenyewe. 
Fikiria hizo timu pamoja na ukwasi walio nao, wangeweza kumiliki makocha kutoka nje ya bara la Afrika. 

Hapa tuna la kujifunza, hata vilabu vyetu nchini inabidi kuhamia huko. Tuwekeze kwa makocha hawa waafrika. 

 Nadhani kuna muunganiko mkubwa na falsafa na utamaduni wa soka la Afrika. 
TANGAZA NASI KWA GHARAMA NAFUU TUPIGIE 0679663340

No comments