𝗡𝗜𝗣𝗢 𝗧𝗔𝗬𝗔𝗥𝗜 𝗞𝗨𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗔 𝗧𝗜𝗠𝗨:- 𝗠𝗔𝗧𝗢𝗟𝗔
⚽ BAADA ya uongozi wa Simba kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco, Kocha msaidizi Seleman Matola amesema yupo tayari kuiongoza timu hiyo mpaka mwisho wa msimu.
⚽ Kocha huyo amesema ujuzi aliochota kutoka kwa makocha wengi aliofanya nao kazi akiwa timu hiyo pamoja na uzoefu wake kwenye ligi ya Tanzania Bara, vinampa kiburi cha kuamini anaweza kufanya kazi hiyo.
⚽"Naushukuru uongozi wa Simba, kwa kunipa nafasi hii ya kuiongoza timu katika nafasi ya kocha mkuu kwa mechi tano zilizobaki kabla msimu kumalizika.Nipo tayari kubeba jukumu hili kutokana na uzoefu niliokuwa nao, cha msingi ni sapoti kutoka kwao na mashabiki pia," amesema Matola.
⚽ Matola amesema hawezi kuzungumzia maamuzi yaliyofanywa na uongozi wa timu ya kumfuta kazi bosi wake Pablo Franco sababu hilo halimhusu.
⚽ Amesema kitu cha msingi kwa sasa ni kuanza mikakati ya kuijenga timu ili msimu ujao irudi kwenye ushindani na kurudisha mataji yote ambayo imeyapoteza msimu huu.
Post a Comment