AMKA NA BWANA LEO 04/06/2022

KESHA LA ASUBUHI 

JUMAMOSI, JUNI 4 2022

MFUATISHE KRISTO NA MAADILI YAKE 

Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu. Wafilipi 2:4, 5.

⏯ Maadili yanayofundishwa na Biblia yanathibitisha kuwa hakuna kiwango kingine bali ukamilifu wa fikra za Mungu, na mapenzi ya Mungu. Mungu anataka kutoka kwa viumbe Vyake ukubali wa Mapenzi Yake. Ukosefu wa tabia ni dhambi, na dhambi ni uasi wa sheria. Sifa zote za tabia ya haki hukaa ndani ya Mungu kwa uwiano mkamilifu kabisa. Wale wote wanaompokea Kristo kuwa Mwokozi wao binafsi wana fursa ya kuwa na sifa hizi. Hii ni sayansi ya utakatifu.

⏯ Uwezekano wa utukufu mkubwa umewekwa mbele ya jamii iliyoanguka! Kupitia Mwana Wake, Mungu amefunua ubora ambao wanadamu wanaweza kufikia. Kupitia kwa tabia njema ya Kristo, wanainuliwa kutoka kwenye hali yao ya ukengeufu, wanatakaswa, na kufanywa wa thamani zaidi kuliko kipande cha dhahabu ya Ofiri. Inawezekana kwao kuwa rafiki wa malaika katika utukufu, na kuakisi sura ya Yesu Kristo, kuangaza hata katika utukufu angavu wa kiti cha enzi cha milele. Ni fursa yao kuwa na imani ambayo kupitia uwezo wa Kristo watafanywa kutokufa. Lakini ni nadra sana wanatambua ni kwa kimo gani wanaweza kukifikia ikiwa watamruhusu Mungu kuwaongoza kila hatua!

⏯ Mungu anamruhusu kila mwanadamu kudhihirisha hali ya upekee. Hataki hata mtu mmoja kuzamisha fikra zake kwenye akili ya mwanadamu mwingine. Wale wanaotamani kubadilishwa katika akili na tabia hawapaswi kulitazamia hilo kwa watu wengine, bali kwake Yeye aliye Mfano wa uungu....

🔘 Kama mfano kwa ajili yetu tunaye Mmoja aliye yote katika yote, aliye mkuu kati ya elfu kumi, Yeye ambaye uzuri wake hauna mfano. Kwa neema alitoa maisha Yake kuwa ya kuigwa na ulimwengu wote. Utajiri na umasikini viliungana katika Kristo; vilevile utukufu na fedheha; nguvu isiyo na kikomo, na upole na unyenyekevu ambavyo vitaakisiwa katika kila nafsi inayompokea. Ndani Yake, kupitia sifa na nguvu za akili ya mwanadamu, hekima ya Mwalimu Mkuu kabisa aliyewahi kujulikana ulimwenguni ilifunuliwa.-Signs of the Times, September 3, 1902.

MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

⏯⏯
MORNING DEVOTION 

SATURDAY, JUNE 4 2022

IMITATE JESUS AND HIS ETHICS 

Let each of you look out not only for his own interests, but also for the interests of others. Let this mind be in you which was also in Christ Jesus. Philippians 2:4, 5, NKJV.

⏯ The ethics inculcated by the gospel acknowledge no standard but the perfection of God's mind, God's will. God requires from His creatures conformity to His will. Imperfection of character is sin, and sin is the transgression of the law. All righteous attributes of character dwell in God as a perfect, harmonious whole. All those who receive Christ as their personal Savior are privileged to possess these attributes. This is the science of holiness.

⏯ How glorious are the possibilities set before the fallen race! Through His Son, God has revealed the excellency to which human beings are capable of attaining. Through the merits of Christ, they are lifted from their depraved state, purified, and made more precious than the golden wedge of Ophir. It is possible for them to become companions of the angels in glory, and to reflect the image of Jesus Christ, shining even in the bright splendor of the eternal throne. It is their privilege to have faith that through the power of Christ they shall be made immortal. Yet how seldom they realize to what heights they could attain if they would allow God to direct their every step!

⏯ God permits every human being to exercise individuality. He desires no one to submerge his or her mind in the mind of a fellow mortal. Those who desire to be transformed in mind and character are not to look to others, but to the divine Example....

🔘 As our Example we have One who is all and in all, the chiefest among ten thousand, One whose excellency is beyond comparison. He graciously adapted His life for universal imitation. United in Christ were wealth and poverty; majesty and abasement; unlimited power, and meekness and lowliness which in every soul who receives Him will be reflected. In Him, through the qualities and powers of the human mind, the wisdom of the greatest Teacher the world has ever known was revealed. The Signs of the Times, September 3, 1902.

MAY GOD BLESS YOU ABUNDANTLY

No comments