PHILIP MPANGO AWATAKA UHAMIAJI KUWA MAKINI

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akiwa ziarani mkoani Kigoma ameitaka Idara ya Uhamiaji mkoani humo kufanya kazi kwa weledi na umakini pale wanapofuatilia wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume na sheria huku akiwataka kutowadhalilisha wananchi.

Makamu wa Rais ameitaka Idara ya Uhamiaji kukaa na wabunge ili kujadili namna bora ya kuchukua hatua stahiki dhidi ya wale ambao sio raia wa Tanzania na wanaishi nchini kinyume cha sheria badala ya kuwasumbua wananchi kwa kigezo cha kuzaliwa mkoani Kigoma.

Akiwa mkoani Kigoma Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Jana Julai 16, 2021 amezindua Jengo la Ofisi ya Taifa Takwimu mkoa wa Kigoma ujenzi ambao umegharimu shilingi milioni 634 ikiwa ni pungufu ya shilingi milioni 50 kutoka shilingi milioni 684 zilizotolewa kujenga jengo hilo.

No comments