MAKADA 30 WA CHAMA CHA CHADEMA WATIWA MBARONI

Baada Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mhe. John Pambalu kuthibitisha asubuhi ya leo Julai 17, 2021, tukio la Jeshi la Polisi kuzingira Boma Hotel, na kumkamata Naibu katibu Mkuu Bavicha taifa Mhe. Yohana Kaunya na Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Mwanza Mhe. Boniface Nkobe.

Jeshi hilo la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia makada 30 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA waliokamatwa baada ya kuvunja mkutano wa kujadili katiba mpya, ulioandaliwa na BAVICHA kwa madai haukuwa halali. 

Hata hivyo BAVICHA imesema huo ulikuwa mkutano wa ndani na haukuhitaji kibali cha polisi.

Binago TV, tuliweza kufika eneo la tukio kuweza kujua nini kinaendelea, lakini RPC-Mwanza, SACP Bw. Ramadhan Ngh'anzi anasema John Heche na Peter Msigwa walipaswa kutoa taarifa kwake kuwa wanaingia Mwanza na watafanya shughuli zao hapo.

Pichani ni baadhi ya Viongozi ambao walihudhuria katika Kongamano la kudai Katiba Mkoani Mwanza leo.
#BinagoUPDATES (ntawiharaphael)✍

No comments