GEKUL APONGEZA WAHITIMU KUCHAGUA SOMO LA MICHEZO

Naibu Waziri Gekul apongeza wahitimu kuchagua Somo la Michezo

Ametoa pongezi hizo Julai 17, 2021 wakati akiwatunuku Vyeti wahitimu katika Chuo hicho

"Nawapongeza wahitimu kwa kuchagua kusomea michezo, huku ni kuona umuhimu wa michezo katika taifa letu na kumuunga mkono Mhe.Samia Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" amesema Mhe.Gekul

Ameongeza kuwa Michezo ni muhimu sana katika taifa ukizingatia  sasa hivi magonjwa mengi yanashamiri ikiwemo UVIKO 19, tunasisitizwa kufanya  mazoezi Hivyo michezo ni afya, na ajira na  inainua uchumi wa taifa letu, hivyo tasnia hii siyo ya kupuuzwa ndiyo maana Mhe. Rais amekuwa akiipa kipaombele sekta ya michezo.

Mhe.Gekul amesema  Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara hiyo imezingatia sana michezo na imetenga fedha nyingi katika sekta hili kuhakikisha inasonga mbele.

"Serikali imeshatoa shilingi 300 milioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya chuo na mwaka huu wa fedha zitatolewa bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa sports academy. Hivyo serikali inaendelea kuwekeza katika michezo kwakuwa ndiko sehemu vijana wetu wataweza kupata ajira kupitia vipaji vyao"amesisitiza Mhe.Gekul.

Amesema kuwa kuna fursa nyingi kamikaze michezo zinajitokeza, kwa sasa wizara hiyo  kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais –TAMISEMI imetenga shule maalum mbili katika kila Mkoa kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya michezo aidha, serikali imeanzisha taasisi za ufundishaji michezo katika kidato cha tano na sita, hizi ni baadhi ya fursa zilizopo hivyo katika kuhitimu mafunzo tutahitaji kuwa na wataalamu katika maeneo hayo.

No comments