GRACE AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Grace Mushi maarufu mtaani kwao kwa jina la Neema kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake Hamis Abdallah ‘Zungu’ ambaye alimmwagia Petroli akiwa ndani kisha kumchoma moto.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea Mbezi Makabe kwa Mzungu.

"Muda wa saa 8:30 usiku Mtuhumiwa huyu alimfungia ndani ya nyumba Hamis akammwagia mafuta ya Petrol na baadaye akachoma moto kitu kilichosababisha Hamisi kufariki”

“----->Hamis alikua ni Rafiki yake wa kiume (Boyfriend), Mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi tukamkamkata na uchunguzi umebaini kulikuwa na mgogoro mkubwa wa kimapenzi kabla kufanyika kwa tukio hili la Kikatili”----- Kamanda ACP Muliro Jumanne Muliro.

Majonzi yametawala Mbezi Makabe Dar es Salaam baada Msichana aiwate Grace Mushi maarufu kama Neema kudaiwa kumuua Boyfriend wake aitwae Hamis maarufu Zungu kwa kuichoma kwa petroli nyumba aliyokuwemo.

Aidha Binago TV imeweza kufika pia eneo la tukio na kuzungumza na mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni Mpangaji katika nyumba hiyo iliyochomwa moto.

"Nilikuwa nimelala nikashtuka mida ya saa 7 nilitaka kwenda chooni, nikaona mlangoni kuna uwazi kama unaingiza mwanga kwa ndani, nilivyofungua mlango nikaona moto umetanda karibia na chumba changu nikaanza kupiga kelele”

“Nikauliza kuna nini mbona moto unawaka, ndio yule Kaka Zungu akaanza kusema Mama Su nipo naungua ndani huku moto umewaka nikamuuliza kuna nini Zungu akanambia Neema kanifungia mlango, nikamwambia fungua mlango akasema siwezi kufungua”

“Ilibidi nianze kufanya ustaarabu wa kumtoa mtoto wangu, nikwambia ngoja nitoke nje niombe msaada wa Watu kuja kunisaidia maana peke yangu siwezi akanijibu sawa Mama Su fanya haraka”----- Shuhuda. 

No comments