🚨 INONGA, CHAMA NA SAIDO WAPELEKWA KWA SELEMAN KOVA, KAMATI YA NIDHAMU
Inaelezwa kuwa Viongozi wa klabu ya Simba wamewapeleka Wachezaji Inonga Baka, Saido Ntibazonkiza na Clatous Chama katika kamati ya nidhamu ya timu hiyo iliyochini ya aliyekuwa kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Seleman Kova, kufuatia madai ya kuhujumu timu katika mchezo wa ligi dhidi ya Yanga.
Kupitia gazeti la Champion, CEO wa Simba Imani Kajula amesema Simba haifanyi jambo kwa kukurupuka na Kila sehemu ina kamati mbali mbali ikiwemo uchunguzi au nidhamu.
Kajula amesema fununu zinazoendelea kuhusu wachezaji hao wachezaji zinafanyiwa kazi na watapelekwa katika kamati ya nidhamu.
"Zile fununu au tetesi za nyota hao tayari zinafanyiwa kazi na kamati itakuja kutolea majibu endapo itabainika kuna makosa". Alisema Kajula
Via Gazeti la Championi, Toa maoni ⚽🔥
Post a Comment