SIMBA ATAJIFUNZA SASA KUCHEZA NA TIMU ZILIZIPO CHINI YAO KWA UKUBWA
Ogopa sana kupigana na mtu ambae anajua wewe ni bora halafu akapata nafasi ya kukupiga.
Mtu anaejua wewe una nguvu ukipigana nae ukajichanganya anaweza kukuua.
SIMBA ni timu ya kudharau mambo walishamfunga goli sita Yanga juzi tu kwenye Club bingwa walimfunga Horoya goli saba7
Lakini matokeo yale yaliishia pale pale uwanjani msimu wa mwaka juzi SIMBA walikuwa hizi goli tano ni kawaida sana kushinda
Coast union alikuja vibaya alipigwa goli nane 8 bado lilikuwa jambo la kawaida sanaa kwao.
Juzi tu wametwaa ngao ya jamii mbele ya mtani wao sijui hata kama mashabiki walifika Air port kupokea ngao.
Wenzao leo goli tano ndo mtaji wao wa kuikuza timu yao na Yanga wana haki ya kujivunia sana
Wao ni timu ambayo ipo chini ya 20 barani Africa kumfunga timu number 8 Africa lazima watambe.
Mamelody ilimfunga goli tano Al Ahly ila kwa sababu Mamelody ni timu kubwa nalo liliishia pale pale uwanjani.
Pata Burudani ya kuangalia Tamthilia na mechi Live na BURE kupitia App yetu ya Binago TV, Bofya hapa ku download 👇🏽
Post a Comment