Moussa Conte kuhitajika Unyamani Simba
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinabainisha kuwa, Kocha Fadlu alivutiwa sana na uwezo wa kiungo mkabaji wa CS Sfaxien, Balla Moussa Conte 🇬🇳 katika michezo miwili waliokutana hapa Dar ambapo Simba ilishinda 2-1 huku Conte akikichafua dakika zote tisini na mchezo wa marudiano uliopigwa Tunis, Simba ikishinda 1-0.
.
Chanzo changu ndani ya Simba kinasema “Baada ya mchezo wa kwanza, Fadlu akataka kujidhihirisha zaidi mchezo wa pili ambapo pia kiungo huyo alicheza dakika zote tisini kwa kiwango kizuri sana,”
.
Chanzo kiliendelea kubainisha kuwa, baada ya mchezo huo wa pili uliochezwa Tunisia wikiendi iliyopita, Fadlu alimpa jukumu kipa wake, Moussa Camara kwenda kuzungumza na Conte ambaye anatoka naye nchi moja ya Guinea.
.
Balla Conte ni kiungo wa ukabaji mzaliwa wa Kamsar nchini Guinea ambaye pia ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo cha ushambuliaji. Kiungo huyo aliyezaliwa Aprili 15, 2004 akiwa na miaka 20 hivi sasa, amekuwa mhimili mzuri ndani ya kikosi cha CS Sfaixien alichojiunga nacho Februari Mosi, 2023, huku malezi yake ya soka akiyapata katika Kituo cha Academie La Louvia kilichopo kwao Guinea.
.
Conte ambaye kiumri bado mdogo, anatakiwa na Fadlu katika kufanikisha projekti yake ya muda mrefu kuijenga timu hiyo kwani tangu ametua Julai 2024, asilimia kubwa ya wachezaji aliowasajili ni chini ya miaka 25, hivyo kiungo huyo ni mtu sahihi kwake kwa faida ya sasa na baadaye.
Post a Comment