SAFARI YA KWANZA YA ATHUMANI KWENDA UWANJA WA FISI.
Athumani, kijana wa miaka 20, mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Usafirishaji (NIT), alikuwa maarufu kwa utulivu wake. Wanafunzi wenzake walimwita “Mzee wa Notes” kwa sababu ya bidii yake darasani.
Lakini, maisha ya hosteli yalimpa changamoto. Marafiki zake, ambao walikuwa na uzoefu mkubwa wa "kutembea usiku," walimshawishi siku moja afanye kitu tofauti.
“Bro, hujawai kwenda Uwanja wa Fisi? Hapo ndo unajua maisha halisi,” alisema Mwakalebela, rafiki yake wa karibu, huku wakicheka kwa nguvu.
Baada ya msukumo wa muda mrefu, Athumani alikubali. Usiku wa Jumamosi ya Januari 2024, walijikusanya na kwenda Uwanja wa Fisi kwa bodaboda. Athumani, akiwa na mhemko mchanganyiko wa hofu na msisimko, alivaa koti lake jipya la jeans na viatu vya raba vya rangi nyeupe. "Bro, unajua leo naenda kufungua ukurasa mpya," alisema, huku marafiki zake wakimcheka kwa kejeli.
Walipofika, Athumani alishangazwa na hali ya eneo hilo. Muziki wa taarab, sauti za wanawake wakipaza sauti kuwavuta wateja, na harufu ya nyama choma vilimkaribisha kwa mshangao. "Ndio hapa Uwanja wa Fisi?" aliuliza kwa sauti ya kutoamini.
Mwakalebela, akicheka, alimwonyesha mwanamke mmoja mwenye mavazi ya kung'aa. “Huyo ndo mzuri kwa beginner kama wewe.” Athumani, akitetemeka kidogo, alimsogelea mwanamke huyo.
"Shikamoo dada," alisema Athumani kwa heshima isiyo ya kawaida kwa mazingira yale. Mwanamke alitabasamu kwa mshangao na kumjibu, “Shikamoo tena? Hapa hatufanyi salamu za nyumbani. hapa ni kutombana kwenda mbele kijana”
Athumani, akijitahidi kujikaza, aliuliza kwa sauti ya chini, "Sasa tunaanzaje?" Mwanamke alimtazama kwa muda na kicheko cha dharau kikavunja ukimya. "Wewe ni mpya, eh? Shida yako ya kwanza ni uoga. Tutaanza kwa kukufundisha jinsi ya kuwa huru."
Marafiki zake walikuwa wakimwangalia kwa mbali huku wakivunjika mbavu kwa kicheko. Athumani alikubali kwenda kwenye kibanda kimoja cha karibu, lakini kabla hawajaingia, ghafla taa za gari la polisi zilionekana. "Polisi! Polisi!" kila mtu alikimbia huku na huku.
Athumani, kwa hofu na kutokujua pa kukimbilia, alijificha chini ya meza ya nyama choma. Polisi walipita huku wakimulika tochi, lakini hawakumuona. Baada ya dakika tano za taharuki, Mwakalebela alimvuta kutoka mafichoni.
“Bro, pole! Hii ndiyo graduation yako ya kwanza,” alisema huku akimcheka. Athumani, akiwa amechafuka na harufu ya nyama choma, alirudi hosteli akiwa ameapa kwamba hatarudi tena Uwanja wa Fisi.
Siku iliyofuata, hadithi yake ilisambaa chuo kizima. Athumani alikuwa shujaa wa "darasa la Uwanja wa Fisi," na marafiki zake waliendelea kumcheka kwa jinsi alivyoanza salamu za "Shikamoo" kwa kahaba.
Post a Comment