MAKALA YA N'GOLO KANTE


 NYAKATI NGUMU NA HISIA ZA UWAJIBIKAJI.


Kuanzia umri mdogo,hisia ya uwajibikaji ilimpata kifo cha baba yake kilimuacha mama wa Ngolo Kante na mzigo mzito wa malezi


alijua thamani ya kufanya kazi kwa bidii kwa sababu aliona hiyo ndiyo njia pekee ya kufikia kitu katika Maisha Kama mzoaji taka Kante alitembea kilomita nyingi kuzunguka Vitongoji vya mashariki mwa Paris akitafuta taka alizikusanya na kuzipeleka kwa makampuni madogo ya kuchakata [recycling] tena, haya ndio yalikuwa maisha yake.


Kante alitafuta njia mbadala za uhuru wa kifedha ili kuinusuru familia yake. Wakati wa kombe la dunia 1998 likiendelea Ufaransa, mashariki mwa Paris akitafuta taka alizikusanya na kuzipeleka kwa makampuni madogo ya kuchakata [recycling] tena, haya ndio yalikuwa maisha yake.


Kante alifanikiwa kupata fedha nyingi hii ilitokana na kukusanya Taka zilizoangushwa na mashabiki wa kandanda kwenye viwanja.


Alikusanya taka nyingi katika uwanja unaotumika kwa mashindano ambayo ni karibu na nyumbani kwake, ikiwa ni pamoja na viwanja vya Hoteli ambazo zilikuwa kama vituo. N'Golo Kante alifanya haya yote ili kupata pesa ambazo aliwekeza katika kitu cha thamani


Baada ya Kombe la Dunia la Ufaransa 98, Kante aliona Ufaransa ya tofauti. Aliona nchi iliyojaa fursa baada ya kuona wachezaji wengi walioibeba Ufaransa wengi wageni ulikuwa wakati ambapo aliwafahamu wahamiaji Waafrika ambao waliisaidia Ufaransa kutwaa kombe la dunia la FIFA la 1998, Thierry Henry, Zinedine Zidane, Patrick Vieira, Lilian Thuram, na Nicolas Anelka. Kombe la Dunia la Ufaransa mnamo 1998 lilileta mabadiliko kwa Ngolo Kante.



Muda mfupi baada ya Kombe la Dunia la 1998, Kante mwenye umri wa miaka 8 alitamani kuchukua soka kama taaluma yake, baada ya kugundua kuwa kuna academy nyingi za soka zilikuwa zimejitokeza karibu na nyumbani kwake haikuchukua muda na safari yake ikaanza kwenye klabu ya JS Suresnes katika viunga vya magharibi mwa Paris.


Kwa sasa Kante anapokea kiasi cha €100m kwa mwaka sawa na Tshs 272.2B


Safari Haikuwa Rahisi kwa wazazi wa kante na kante mwenyewe kutoka Mali mpaka Ufaransa Nyakati Ngumu zinahitaji Imani na kama hakuna imani basi hakuna subira. 📝🙏🏼

No comments