AMKA NA BWANA LEO 24

KESHA LA ASUBUHI

Jumanne 24/08/2021

*SHIKILIA NGUVU ZA MUNGU*

*Ndipo ulipowaambia watakatifu wako Kwa njozi. Ukasema, nimempa aliye hodari msaada.* *Zaburi 89:19*

Bwana anakupenda. Bwana ni mwenye huruma nyingi. Ahadi yake ni, *"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi" (Yakobo 4:8)*. Adui atakapokuja kama mafuriko, Roho wa Bwana atainua juu kwa ajili yako bendera dhidi yake. *Kumbuka kwamba Yesu *Kristo ndiye tumaini lako. Katika mambo ya kusikitisha na kukatisha tamaa yatakayokujia wakati wowote, Kristo anakumbia, *"Au azishike nguvu zangu, afanye amani nami; Naam afanye amani nami" (Isaya 27:5).*

Kazi yako ni kuishikilia nguvu Ile iliyo thabiti kama vile kilivyo kiti Cha enzi Cha milele. *Mwamini Mungu. Mtumainie yeye. Uwe mchangamfu Katika Hali zote. Ijapokuwa unaweza kiwa na majaribio, fahamu kwamba Kristo alipata mateso haya Kwa niaba ya urithi Wake*. Hakuna kitu ambacho ni cha thamani kubwa Kwa Bwana kama Kanisa Lake. Bwana huangalia moyo. Anawajua walio wake. Bwana ataijaribu na kuithibitisha Kila nafsi inayoishi. "Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; Bali wabaya watatenda mabaya; Wala hawataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndiowatakaoelewa" (Danieli 12:10).

*Hebu wale wanaompenda Mungu na ni watendaji wa neno Lake waimbe sifa na Shukrani badala ya kusema maneno ya kulaumu, ya kutafuta mkosa, na ya kunung'unika*. Bwana atawabariki wale wanaochangia kuleta amani. *Mtumainie Bwana. Usiruhusu hisia, kauli, au mtazamo wa wakala yeyote wa kibinadamu kukufadhaisha*. Kuwa mwangalifu kwamba Kwa maneno au matendo usiwape wengine fursa yeyote ya kupata faida ya kukusononesha. *Dumu kumtazama Yesu. Yeye ni nguvu yako. *Kwa kumtazama Yesu utabadikishwa kufanana naye. Atakuwa afya ya uso wako na Mungu wako.*

*Kanisa linakuhitaji, na inahitajika kulainisha na kutiisha hisia zao mwenyewe Kwa ajili ya Kristo. Anataka Roho Mtakatifu wake akutendee kazi. Ndipo utakapoweza kutoa maisha na faraja Kwa kanisa. Hebu maneno yako na yachaguliwe vyema ili upate kuwa baraka ya kweli kwa kanisa. Msizitese nafsi zenu Kwa sababu ya wengine kutofuata utaratibu. Mjitawale wenyewe, na mwe waaminifu katika mambo yote.*

*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*

No comments