Asubuhi njema
*KESHA LA ASUBUHI.*
Ijumaa, 29/07/2022.
*TUMIA MUDA KWA MAOMBI NA KUSOMA NENO.*
*Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikialo lile neno, na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. Marko 4:18, 19.*
✍️ Kristo alibainisha mambo ambayo ni hatari kwa nafsi. Kama ilivyoandikwa na Marko, Anataja shughuli za dunia hii, udanganyifu wa mali, na tamaa za vitu vingine. Luka anabainisha masumbuko hayo, utajiri, na anasa za maisha haya. Haya ndiyo hulisonga neno, ile mbegu ya kiroho inayokua. Nafsi inaacha kuchota lishe kutoka kwa Kristo, na hali ya kiroho inakufa moyoni.
✍️ "Shughuli za dunia hii." Hakuna tabaka lililo huru kutokana na jaribu la shughuli za kidunia. Kwa maskini, kazi ya taabu, unyimwaji na woga wa uhitaji huleta mashaka na mizigo. Kwa matajiri huja hofu ya kupata hasara na wingi wa mahangaiko. Wafuasi wengi wa Kristo husahau somo ambalo ametuamuru tujifunze kutoka kwa maua ya kondeni. Hawatumainii utunzaji Wake wa kila mara. Kristo hawezi kubeba mzigo wao, kwa sababu hawamtwiki Yeye....
✍️ Wengi ambao wangeweza kuzaa matunda katika utumishi wa Mungu hudanganyika katika kujipatia mali. Nguvu zao zote humezwa katika shughuli za kibiashara, na wanajihisi kuwajibika kiasi cha kupuuza mambo ya kiroho. Kwa kufanya hivyo wanajitenga na Mungu.... Tunapaswa kufanya kazi ili tuwagawie wenye mahitaji. Wakristo lazima wafanye kazi, lazima wajihusishe na biashara, na wanaweza kufanya hivyo bila kutenda dhambi. Lakini wengi wanajishughulisha sana na biashara kiasi kwamba hawana muda wa maombi, hawana muda wa kujifunza Biblia, hawana muda wa kumtafuta na kumtumikia Mungu.
✍️ Wakati fulani matamanio ya nafsi ni kutafuta utakatifu na mbingu; lakini hakuna muda wa kugeuka kando kutoka kwa kelele za ulimwengu ili kusikiliza matamshi makuu na yenye mamlaka ya Roho wa Mungu. Mambo ya umilele yanafanywa kuwa chini, na mambo ya ulimwengu kuwa makuu. Haiwezekani kwa mbegu ya Neno kuzaa matunda; kwani uhai wa nafsi unatolewa ili kurutubisha miiba ya kidunia.
✍️ *Na wengi ambao wanafanya kazi kwa kusudi tofauti sana huanguka kwenye kosa kama hilo. Wanafanya kazi kwa manufaa ya wengine; majukumu yao yanasonga, majukumu yao ni mengi, na wanaruhusu wafanya kazi wao kuzuia ibada.... Wanatembea mbali na Kristo, maisha yao hayajaingiliwa na neema Yake, na tabia za ubinafsi zinafichuliwa.*
*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA.*
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment