Kocha Mexime kachambua usajili wa klabu za Yanga na Simba SC.
"Huwezi kuubeza usajili wa Yanga kama unaakili timamu. Klabu ya Yanga imefanya usajili wa kimbinu kuzingatia zaidi uweledi na sio ushamba kuonekana unajaza Wachezaji wasio na faida"
"Watazame Yanga kwa jicho la tatu utagundua kwanza wamepitisha panga 🗡️ hasa kwa kuwatoa wachezaji wasioendana na falsafa ya mwalimu (Kocha), pia wachezaji wengine walikuwa mizigo tu kwa klabu bila sababu"
"Watazame Simba SC, hawajui hata wanalofanya, kuna wachezaji pale rundo na ambao msimu uliomalizika hakuna la maana walilolifanya, wamechoka na wamezeeka na Simba wenyewe wanajua hilo ila wanavigugumizi, eti kuvunja mikataba wanashindwa, ni ubabaishaji tu kwenye soka"
"Kuwaacha waendelee kikosini Wachezaji waliokosa mipango ni hatari sana, hawa ndio huwa wanageuka wachawi kuroga Wachezaji vijana wanao perform ili wapate nafasi ya kucheza"
"Nimecheza mpira nayajua haya, siongei kufurahisha genge bro, Simba wanatafuta mchawi na wanatapatapa kwa sababu ya kurundika mizigo pale,, Yanga huo ujinga wameachana nao na ukiwatazama unawaona kabisa wanaelekea wapi, ndio soka la kisasa linataka mipango kama hiyo"
"Unaanzaje kumponda Bigirimana ! Kacheza Ulaya EPL 🏴 sio wa kawaida huyo anakitu tazama yule beki Mutambala ametajwa kwenye kikosi bora cha (CAF) miaka kadhaa nyuma hao ni baadhi tu"
"Sasa angalia Simba, timu iko pre season bado unafanya 'Ana ana doo' za usajili, lini timu ita concentrate na program za mwalimu ?!"
🔍 Mecky Mexime
Post a Comment