AMKA NA BWANA LEO 16/10/2023


 KESHA LA ASUBUHI 2023 


JUMATATU, OKTOBA 16 


MFALME WA UZIMA 


Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. -Mathayo 4:23


🔰 Juu ya wote wanaojihusisha na kazi ya Bwana umewekwa wajibu wa kutimiza agizo: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:19, 20).


🔰 Kristo Mwenyewe ametupatia mfano wa jinsi tunavyopaswa kufanya kazi. Soma sura ya nne ya kitabu cha Mathayo, na ujifunze ni mbinu zipi ambazo Kristo, Mfalme wa Uzima, alizifuata katika ufundishaji Wake. "Akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali, ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia" (Mathayo 4:13-16).


🔰 "Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata" (Mathayo 4:18-22). 


🔰 Hawa wavuvi maskini walikuwa wanafunzi wa kwanza wa Kristo. Hakusema kuwa wangepokea kiasi fulani cha pesa kwa huduma zao. Iliwapasa kushiriki Naye kujikana nafsi na kujitoa Kwake kafara..


🔘 Katika kila namna iliyowezekana Kristo alikuwa mmishenari daktari. Alikuja katika ulimwengu huu kuhubiri injili na kuponya wagonjwa. Alikuja kama mponyaji wa miili na roho za wanadamu. Ujumbe Wake ulikuwa kwamba utii kwa sheria za ufalme wa Mungu ungewaletea wanaume na wanawake afya na mafanikio.-Counsels on Health, uk. 316, 317.


Tafakari Zaidi: Je, nimeshajifunza hata kidogo mbinu ambazo Yesu alizitumia kuhudumia mahitaji ya kimwili na kiroho ya watu waliopotea? Ninawezaje kujifunza kutokana na jinsi alivyofanya kazi?


MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA


Tafadhali Subscribe, Like, Share YouTube channel yetu ya 👉🏽 Binago TV

No comments