MR.BLUE ATHIBITISHA KUWA MKEWE ALIMTOA KWENYE MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA


 Mwanamuziki wa Bongofleva Herry Sameer Rajab almaarufu kama #MrBlue amefanya mahojiano na BBC na kufunguka kuwa kuna kipindi alipotea kwenye muziki kutokana na starehe na kujiingiza kwenye dimbwi la matumizi ya dawa za kulevywa huku akimtaja mke wake kuwa ndiye aliyemsaidia kumtoa kwenye changamoto hiyo.


“Mimi mke wangu namshukuru sana kwani yeye ndio amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kubadilika, alikuwa ananiambia taratibu vitu vya kufanya na badaye aliposhika ujauzito ndio nikagundua naenda kuwa na familia” – ameelezea Mr. Blue.


“Mimi wakati naanza muziki nilikuwa mtoto na sikuwa na rafiki lakini watu walikuja wakijifanya wananijua wamesoma na mimi kwahiyo ule ushkaji mtu akichoma na mimi nachoma, mara pombe nikawa siendi studio, mimi nimeharibiwa na watu waliokuja baada ya mimi kuwa staa” – Mr.Blue.

No comments