π¨ ππΌππΌππ ππΎπππΎππππ ππππΌπΌπππΌ
Mchambuzi Jemedari Said amjia Juu Mbunge wa Singida kutembelea kambi ya timu inayoishi Singida.
"MDHAMINI WA YANGA KAMBINI KWA IHEFU SIKU CHACHE KABLA YA MECHI KATI YAO INATIA MASHAKA."
"Waziri wa Fedha wa Tanzania Mh. Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea kambi ya timu ya IHEFU ambayo inajiandaa kucheza na Yanga SC hapo tarehe 17 Machi 2024 uwanja wa Azam Complex Chamazi."
"Mwigulu ni Mwanamichezo na Mwanachama wa klabu ya Yanga aliye pia Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Klabu hiyo Kongwe na kubwa nchini, wajumbe wengine ni Anthony Mavunde ambaye ni Waziri wa Madini wa Tanzania na George Huruma Mkuchika ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalumu."
"Kumekuwa na maneno kwamba klabu ya IHEFU imeuzwa kutoka kwa wamiliki wake na sasa imenunuliwa Mkoani Singida na ndiyo maana imehamia uwanja wa CCM Liti na kuacha uwanja wa zamani wa Highland Estates. Mwigulu pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi Jimbo ambalo liko Mkoani Singida."
"CEO wa Bodi ya ligi ndugu Almasi Jumapili Kasongo alipoulizwa kuhusu timu ya IHEFU kuuzwa na kumilikiwa huko Mkoani Singida alisema HAJUI kuhusu hilo na akataka tusiishi kwa hofu na dhana, tunamuomba asome alama za nyakati lakini pia ni hatari kwa namna mpira wetu unavyoendesha kama Afisa Mtendaji Mkuu kuna mambo yanampita na hayajui kabisa kabisa."
"Pichani Mh Mwigulu alkipozi kupiga picha na baadhi ya wachezaji wa IHEFU katika kile kilichoelezwa kutoa hamasa kwa timu hiyo ambayo inacheza na timu yake ya Yanga. Kikatiba Bodi ya Wadhamini (Trustees) ndiyo wenye mali. Mpira wetu una mwendo mrefu kufikia UELEDI WA KWELI tuambiane ukweli hatakama unauma, hii sio sawa kwa mdhamini wa timu kwenda kwenye kambi ya timu inayocheza na timu yako, inatengeneza mashaka makubwa, tuweke hisia kando"
©️ Jemedari Said
Post a Comment