MIAKA 22 YA MFUKO WA AFYA YA PAMOJA NA MAFANIKIO YAKE
Naibu Waziri Ofisi Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ameweka wazi mafanikio yaliyopatikana katika miaka 22 ya Utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Pamoja (Health Busket Fund) ikiwa ni pamoja kuimarisha miundombinu ya sekta ya afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
Akifafanua katika Mkutano wa Ngazi za juu na Maadhimisho ya Miaka 22 ya Mfuko wa Afya ya Pamoja uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es salaam, Dkt. Dugange amesema mafanikio hayo yamepewa nguvu na upelekekaji wa Fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya (Direct health Facility Financing- DHFF) ambao umeleta tija na kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwenye ngazi ya jamii.
" Mfuko wa Afya ya Pamoja umeleta mafanikio mengi katika sekta ya afya, kumekuwa na maboresho makubwa katika ujenzi na ukarabati Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, ajira, upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba."
Aisha, Dkt Dugange amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wadau wanaochangia Mfuko wa Afya wa Pamoja (HBF) na katika kuadhimishia miaka hii 22 ni vyema kuangalia namna ambavyo tunaweza kuendelea na mfuko huu kwa mafanikio ikiwa ni pamoja na wadau wengine kuendelea kujiunga.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 90 za Fedha za Mfuko wa Afya ya Pamoja zinepelekwa moja kwa moja kwenye Halmashauri zetu ambapo mpaka sasa tuna Halmashauri 184, Hospital za Halmashauri 155, Hospitali teule 86, Vituo vya Afya 607 na Zahanati 5152 ambazo zinanufaika moja kwa moja kupitia Mfuko wa Afya ya pamoja.
"Kwa hakika miaka hii 22 ya utekelezaji na usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Pamoja tunashuhudia mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za Afyamsingi na namna ambavyo huduma zimefika kwenye maeneo magumu kufikika ambako sasa jamii inanufaika na huduma bora za afya kupitia uwezeshaji wa mfuko."
Dkt Dugange alioongeza:" tumefanikiwa kukarabati na kuwezesha vituo vya afya kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa wakinamama wajawazito na mpaka sasa Vituo vya Afya 244 kati ya 304 vimewezeshwa kutoa huduma hii na wakinamama zaidi ya 34,000 wanapatiwa huduma za upasuaji wa dharura

Post a Comment