Rasmi: Yanga imefuzu robo fainali
UKIJAA TU KWENYE MFUMO ....... utaenda kuhadithia .!
✍🏻Performance ya hali ya juu sana , kila mchezaji katoa 100% yake uwanjani , ufundi , mbinu , umakini ( yes hii ya umakini ngumu kuwa 100% Binadamu hao ) , Yanga SC walihitajika ku turn up na wamwwapa mashabiki wao ladha ya " PACOME DAY "
✍🏻Gamondi alifanya kile ambacho kocha unatakiwa kufanya " wachezaji wako wakae kwenye nafasi hatarishi kwa mpinzani " . Aziz , Pacome na Maxi ni lazima :-
1: Wacheze karibu karibu sana , ili kufanikisha madhara kwenye mita 25 za mwisho
2: Hakikisha wanakuwa katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo wa timu pinzani ( between the lines )
3: Ili kufanikisha hili inahitaji wachezaji wanne takribani watano wafanye kazi zao kwa ufanisi , ambao ni :-
A: Fullbacks wawe wana overlap pembeni ili kufanya Pacome na Aziz kuwa ndani zaidi
B: Mshambuliaji ambao sio static yani yule anayesimama tu bali anayefanya sana runs , kwanini kuwahamisha mabeki wa kati wa timu pinzani
C: Mudathir kufanya sana forward Runs :inahitaji energy ya hali ya juu sana , akifanya hivyo maana yake anateka akili ya viungo wa timu pinzani
D: Aucho passing kupita kwenye mistari hasa mstari ule wa kiungo wa timu pinzani
Na Yanga leo walifanya hivyo vitu kwa umakini wa hali ya juu sana na ufanisi sana.! Gamondi lazima ajivunie .
✍🏻CRB leo hawatokuwa na lawama , kuna ambacho unafanya kwa usahihi halafu kuna mpinzani wako kuwa bora zaidi katika siku husika , spaces walizokuwa wanaziacha leo ziliadhibiwa kwa ufanisi zaidi na pengine watajiona wana bahati sana ya kuruhusu 4-0 pengine ingekuwa 6 au 7 ... ni hatari kuwapa wachezaji wazuri muda na nafasi kwenye mpira
NOTE
1: Mudathir ile energy yake ni kitu muhimu sana kwa kiungo cha Yanga , runs zake 🔥
2: Yanga , walikuwa wanawababua CRB hata wiki leo kwa nafasi bora walizopata
3: Walinzi wa Yanga na Diarra .. perfect game 🔥
4: Wale three AMIGOS ( Aziz Pacome na Maxi ) wakiwa na mechi nzuri kazi unayo
5: PACOME ... unasema nini kwake ? What a player .! Anacheza na swagga sana , maarifa mengi.!
6: Robo fainali ileeeeeeeee.!
7: CRB wanajua wamefungwa na timu bora uwanjani
FT: Yanga SC 4-0 CRB
CC George Ambangile ⚽️ 🔥
Post a Comment