GSM kakubali kujenga Uwanja wa Yanga SC
Kutoka kwa Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said @caamil_88 amethitibisha kuwa, GSM ameridhia kwa dhati kujenga uwanja ndani ya Makao Makuu ya klabu Jangwani.
Ikiwa klabu ya Yanga inasherehekea miaka 89 tangu klabu hiyo kuanzishwa, habari njema kutoka kwa mfadhili wa Yanga, Mr. Ghalib Said Mohamed, GSM ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young African Sports Club, katika eneo la Makao Makuu ya klabu, Jangwani, Jijini Dar es Salaam.
Hakuna budi kuendelea kumpongeza kiongozi huyu mpenda michezo kwa kuendelea kujitoa kwa dhati katika kuufanya mpira wetu kuwa wenye nguvu.
Toa maoni yako
Post a Comment