MSAFARA WA MAKONDA WAPATA AJALI MASASI
Msafara wa katibu wa nec itikadi uenezi na mafunzo wa Ccm Paul Makonda umepata ajali katika eneo la Masasi mkoani Mtwara
Ajali hiyo iliyotokea saa 9 alasiri imehusisha zaidi ya magari 7 yaliyokuwepo katika msafara wa muenezi Makonda uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea jijini Dar es salaam
Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu wasiopungua 7 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote
Hata hivyo kwa upande wa hali ya kiafya ya katibu wa nec itikadi uenezi na mafunzo wa Ccm Paul Makonda ipo salama.
Post a Comment