IVORY COAST BINGWA AFCON 2023 🏆


 TUZO ZA AFCON 2023 

1: Mchezaji bora wa mashindano - William Troost-Ekong ( NIGERIA)



2: Mfungaji bora wa mashindano - Emilio Nsue ( EQ. GUINEA ) 



3: Golikipa bora wa mashindano - Ronwen Williams ( S. AFRICA ) 





WAFALME WA AFRIKA : IVORY COAST 

✍🏻Timu bora imeshinda mechi , Ivory Coast walikuwa bora kila eneo walifanya vitu vingi sana kwa usahihi , walikuwa wajasiri sana kucheza mechi ya kujiachia , waliamini katika kufunga goli zaidi ya mpinzani 

✍🏻Emerse Fae anastahili pongezi jinsi alivyoi set team yake dhidi ya Nigeria . Lengo lake ni kupata faida ya idadi ya wachezaji katika kila " Phase " ya mchezo ; kuanzia nyuma , katikati na mbele . Alifanyaje ? 

1: Muundo wa 2-3-5 wakiwa na mali na 4-5-1 bila mpira lakini wakiwa na mali ndio ilikuwa stori zaidi 

2: Phase ya kwanza 2v1 mabeki wawili wa kati wa Ivory Coast dhidi ya Osimhen wakienda Phase ya pili ambapo wanakuwa watano ( Fullbacks wawili na Seri katika mstari mmoja na mbele yao Fofana na Kessie dhidi ya wanne wa Nigeria ) Phase ya tatu 5v5 : Nigeria wanazuia kwa watano nyuma na Ivory Coast watatu wa mbele wakiungana na namba 8 wawili wanaotoka kwenye kiungo ( Fofana na Kessie ) . 

3: Baada ya hapo ilikuwa anahitaji ufundi wa wachezaji kuonesha nini wanaweza kufanya wakiwa na faida ya mchezaji au wakiwa sawa kwa idadi . Hapo ndio Adingra , Kessie , Fofana , Gradel walichokuwa wanafanya wakikabiliana hata 1v1  

✍🏻Nigeria sio kwamba walikuwa vibaya bali naamini Ivory Coast waliwalazimisha kuwa hivyo , walipoteza 50/50 nyingi , passing game yao haikuwa nzuri ( pressing ya Ivory Coast ilisababisha hili ) , lakini walishambulia na idadi ndogo sana ya wachezaji mpaka zile dakika 10 za mwisho ambapo kocha wa Nigeria alipoamua kujilipua lakini ilikuwa " TOO LATE " .! 

KIUFUPI : IVORY COAST waliitaka sana mechi zaidi ya Nigeria , hata takwimu tu zinaongea 

NOTE 

1: Ile Battle baina ya Osimhen na Ndicka naamini itaendelea Serie A ( Napoli Vs Roma ) 😀

2: Seri anarahisha vitu kwenye namba 6 kuwasaidia namba 8 wake wawili juu yake 

3: Ekong sitoshangaa kabisa kumuona kwenye kikosi bora cha mashindano 

4: Kessie alionesha kabisa hii mechi anaitaka sana : Powerful 🔥

5: SIMON ADINGRA alikuwa anampika sana Ola Aina , Brighton wajiandae kwa ofa .! Msumbufu na hatari .! 

MASHINDANO BORA KABISA 👏🏻👏🏻🔥🔥

FT: Ivory Coast 2-1 Nigeria CC George Ambangile #binagoupdates #AFCON2023

 

No comments