Alonso hashikiki Bundesliga


 ALONSO MASTERCLASS 


✍🏻Xabi Alonso alipatia kila kitu lakini alihitaji pia ufanisi wa wachezaji wake kuiangamiza Bayern 


✍🏻Leverkusen bila mpira walikuwa na uimara sana, walifanya man to man marking uwanja mzima ... kivipi 


1: Bayern walikuwa na Back 3 ( Upamecano Dier na Kim ) na Leverkusen walikuwa wanzuia kwa 5-2-3 ( Adli Writz na Tella ) ambao walikuwa wanasimama mbele ya Back 3 ya Bayern 


2: Andrich na Xhaka Ambao viungo wawili wa Leverkusen wenyewe wanahakikisha viungo wawili wa kati wa Bayern hawapati mali wakiwa huru . 


3: Leverkusen nao walikuwa na Back 3 yao nyuma ambapo wale wawili wa pembeni walikuwa wanasuburia Bayern wakifanikiwa kufika kati basi haraka wanafika kwa namba 10 wawili wa Bayern ( Sane na Musiala ) huku Tah dhidi ya Kane , Wingbacks Vs Wingbacks . 


4: Leverkusen walifunga space zote za kati na pembeni walikuwa aggressive sana kukabiliana 1v1 


✍🏻Leverkusen wakiwa na mali , unaziona triangles kibao uwanjani kila sehemu ya mpira , bila kuwa na namba 9 halisi , timu yao ilikuwa fluid , mobile sana , wanatembea mno , na naamini aliyewamaliza sana ni Hincapie kwanini ? Yeye alikuwa LCB ( leftsided Centreback kwenye wale back 3 ) lakini Leverkusen wakiwa na mali anakuwa kama beki wa kushoto ili kumruhusu Grimaldo kutoka kuwa wingback mpaka kiungo kama vile namba 10 ambayo iliwapa faida sana Leverkusen nyuma ya kiungo cha Bayern 


✍🏻Kiukweli hata usema uongeze dakika 20 Bayern hawafungi goli , Bayern walikosa suluhisho kabisa ndio maana mechi inaisha wana on target moja tu 



NOTE 


1: Florian Wirtz hana mambo mengi " nipe nikupe " space ipo wapi , anaitumia 


2: Kiukweli ngumu kutaja mchezaji mmoja mmoja Leverkusen wote walikuwa vizuri sanaaaaa 


3: Bayern sasa daah ... kuna nyakati hawakuwa makini pasi mkaa kibao 


4: Hapa sasa Leverkusen washindwe wao wenyewe , gap la point 5 na mechi 13 zimebaki


FT: Leverkusen 3-0 Bayern


CC George Ambangile 

No comments