Mbowe aandamana na watoto wake
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe leo ameongoza maandamano ya amani leo January 24,2024 akiwa ameambatana na Watoto wake wanne ambao ni Aishi, Nicole, Denis na Dudley ambapo Watoto hao wamesema wamejiunga na maandamano hayo kusimama na Nchi yao, kudai haki za binadamu na katiba mpya.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Freeman Mbowe amesema Wananchi wanataabika na bei ya vyakula, umeme, wanataabika na mafuriko na kwamba Serikali haisikilizi Wananchi wakati Watumishi wa Serikali wakilipwa posho nzuri, magari mapya, nyumba za Serikali, umeme wa Serikali, genereta za Serikali.
“CHADEMA tunawahamasisha Watanzania tusimame tupaze sauti zetu ili Serikali itambue kwamba ina wajibu wa kujipanga na kuweka mkakati wa kupunguza gharama za maisha kwa Wananchi wa kawaida, hoja kubwa ya pili ni miswada iliyopo Bungeni ambayo inakosa sifa za kuleta mabadiliko ya mifumo ya kiuchaguzi katika Taifa letu, tunataka miswada iondolewe Bungeni"
“Sisi tutaendelea na maandamano na hayatokoma, yatakuwa Dar es salaam yatakwenda Mikoani kote yatarudi tena Dar es salaam yatazunguka maandamano mpaka siku Serikali itakapoelewa kwamba malalamiko yetu sio ya Mbowe ni ya Watanzania wa Mikoa yote ya Wilaya zote”
CC MillardAyo
Post a Comment