Nilihisi mume wangu ana matatizo


 "Mimi ni mama wa mtoto mmoja nimeolewa, ndoa yangu ina miaka 5 sasa. Katika kuhangaika kutafuta mtoto, nilihisi mume wangu ana matatizo, hivyo ndoa yangu ikiwa na miaka 4 nilimtafuta X wangu kwa lengo la kupata mimba yake kisha nirudi kwenye ndoa yangu kutulia.


Kweli baada ya kurudiana nilibeba mimba yake, nilitaka kumuacha lakini nikajikuta nishaanza kumpenda kwani hata yeye aliniambia bado ananikumbuka kuna mwanamke alikuwa naye wameachana hivyo niliamua kuendeleza mahusiano na X wangu.


Kliniki nililazimika kwenda sehemu mbili tofauti moja nikawa naenda na mume wangu na nyingine nilikuwa naenda na X wangu hivyo nikawa nina kadi mbili za kliniki. Mipango ilikuwa nikishajifungua ndiyo nitafute sababu mume wangu ajue mtoto si wake aniache niolewe na X wangu.


Nikiwa na imani kuwa mimba ni ya X wangu, nilipojifungua mtoto alikuwa ni kopi kabisa ya mume wangu, yaani hauulizi ukimuangalia mpaka kucha ni za mume wangu ni kama alikuwa kajizaa. Kweli nilipaniki kwani nilishaanza kumchukia mume wangu na tulikuwa na mipango mingi na X wangu.



Nimechukua mkopo kazini hivyo mpaka sasa ninakatwa tayari tushanunua kiwanja na X na kuanza kujenga ili nikijifungua tu tunahamia kwetu na nyumba inakaribia kukamilika. Shida inakuja sasa, baada ya X kuona mtoto na kuona kafanana na mume wangu naona kabadilika, hataki tena mambo ya kuendelea na mahusiano.


Hajaniambia kitu lakini namuona kama kapunguza mawasiliano, nimechanganyikiwa kweli sijui nafanya nini. Nimejikuta nampenda sana na nimewekeza sana kwake naomba unisaidie nifanye nini ili amkubali mtoto hata kama si wake.


Sikotayari kuendelea na mume wangu, hajawahi kunifanyia baya lolote ila tu najihisi namchukia na sitaki kuwa naye, ninachotaka tu ni X ajue sikumdanganya na ampende mtoto wet kwani kalea sana hii mimba ni kama damu yake!"


Na IDDI MAKENGO


NISAFISHE 🎵 🔥 is OUT.. Kutazama Bofya 👇🏽

               Nisafishe New Hit song

No comments