Hii ndio maana ya sikukuu ya Krismas "Xmas"

ASILI YA CHRISTMAS.

Mwanzo 10:8

Katika kitabu cha Mwanzo 10:8 tunakuta habari za mtu mmoja maarufu kwa jina anaitwa Nimrod alikuwa mtu maarufu sana katika zama zake. Tena alikua mfalme wa kwanza wa kibinadamu katika Biblia. Nimrod ananenwa kuwa mtu hodari, katika Mwanzo 10:8-12, mwanzo wa ufalme wake ni babeli; Ereku, Akadi, Kalne, Ashuru, akajenga ninawi na Rehobothiri, Kala na kati ya ninawi na Kalanago ilikuwa ni miji mikubwa. Mke wa Nimrod aliitwa Shemiramis.

SIFA ZA NIMROD (NIMRUDI).

A.    Mwenye hekima nyingi.

B.     Mwenye kipaji cha kutawala .

C.     Mwenye ujuzi wa mambo.

D.    Mwenye uwezo na nguvu za kushawishi.

E.     Mwenye mawazo makubwa.

F.      Mwenye uwezo wa kutenda.

G.    Mawazo yake yalikubaklika na watu wote.

H.    Ndiye aliyejenga mji  wa Ninawi na mji wa Babeli.

I.       Alijenga ukuta wa  Babeli kuzungukia mji wote ili kuweza kukomesha tatizo la wanyamapori wakali waliokuwa wakiwasumbua.

J.       Alishawishi watu wajipatie mfalme atakayewaongoza mara baada ya kumaliza kujenga ukuta, na kutokana na uhodari na umaarufu wake wa kudhibiti wanyamapori wakali aliteuliwa na kufanywa kuwa mfalme wa kwanza aliyetajwa na Biblia kwa wanadamu.

K.    Alikuwa ni mfalme asiyemcha Mungu.

L.     Alikuwa ni kuhani wa ibada ya shetani (miungu) na mpagani wa kutisha.

M.   Nimrod kuhai mfalme alikufa.  

N.    Kutokana na umaarufu wake na kwa vile alikuwa mfalme wa kwanza wa taifa hilo, wanadamu waliomboleza sana juu ya kifo chake huko Babeli alikotawala, lakini cha ajabu hata baada ya kifo chake dini ya babeli aliyoianzisha iliendelea hadi leo.

Baada ya miaka ya kifo cha Nimrod, malkia alizini na kuhani wake wa Matambiko katika ibada ya jua. Katika kuzini na kuhani huyo malkia alibeba mimba, kwakuwa alikuwa malkia na hana mume, na huku ana-mimba , watu wake walimuuliza kwamba hii mimba imetoka wapi (ni yanani?) huku huna mume?

Kwa makini na utaratibu malkia alijibu kwamba nilipokua nimeamka asubuhi nilitoka kwenda kuota jua, mionzi ya jua ilinipiga tumboni nikasikia dalili za mimba na mimba ikaanza kukuwa taratibu, shemiramis asingesema uongo huo angeuawa na watu wake kutokana na mila na desturi za watu hawa. Shemiramis alibeba mimba tarehe 25/3…alijifunguwa tarehe 24 kuamkia tarehe 25/12…

SHEREHE YA KUZALIWA KWA TAMMUZ.

Katika asubuhi ya tarehe 25/12…ilikuwa ni sherehe kubwa sana ya kuzaliwa kwa mtoto TAMMUZ, pia iliaminika kwamba huyu mtoto ni mtakakatifu, kwakuwa mimba yake imetokana na mionzi ya jua, pia iliaminika kwamba Nimrod aliendelea kuzaa na mke wake huku akiwa katika jua. Yeremia 7:17-18 inaonyesha sherehe aliyofanyiwa katika kuzaliwa kwake (TAMMUZ),Sherehe hiyo iliridhiwa na wana wa Israel. Wakina baba na akina Mama na watoto wote walijumuika katika maandalizi ya sherehe hiyo kubwa. Yeremia 7:18, yeremia 52:31.

KIFO CHA TAMMUZ.

Hata hivyo mtoto huyu alifariki dunia baada ya kipindi cha miaka mitatu tu. Maombolezo makubwa yalifanyika ili kumuombolezea TAMMUZ. Wazee, wakina mama na watoto wote, waliomboleza kwa machungu sana(Ezekieli 8:14). Shemiramis mke wa Mfalme Nimrod akazua uongo mwingine, kwamba alienda kwa mungu hera, mungu hera alimpa masharti kwamba awakusanye wanawake wote wafunge kwa siku arobaini(40) ndipo ombi lake litafanikiwa. Shemiramis akafanya hivyo akawakusanya wanawake wote na kufunga nao siku 40. Huu ndiyo mwanzo wakwarezma.

MTI WA CHRISMAS(MKRISMAS) NA IBADA YA UMIZIMU.

Katika mashariki ya kati, Neno “T”, ni ishara ya takatifu. Kwani ulikuwa ni mti waliokuwa wakitolea kafara. Maana ya Tammuz ni mungu katika mwili(T-mungu mwili). Walipokuwa wakitoa kafara katika mti huu, uliitwa X-MASS.

Ø  X = hakuna,

Ø  Mass  =  sherehe.

Ø  X + MASS = Hakuna sherehe yoyote.

Mti huo ulioitwa x-mass waliokuwa wakitumia kufanya kafara zao ambapo x-mass ilionyesha hakuna sherehe katika eneo hilo la kufanyia kafara. Watu wote walikaa kimya katika ibada hii ya Miungu. Mti huo leo unaitwa mkrismas(Mti wa chrismas). Lakini pia Makuhani waliokuwa wakihudumu katika ibada hizo za miungu walikuwa wakivaa alama ya “T” shingoni au kwente bega kuonyesha utakatifu. Shetani alifanya mpango, mwana wa Mungu naye akatolewa kafara kwenye mti huu wa LAANA ambao ni ishara takatifu ya shetani Galatia 3:13.

MIUNGU MIKUU:

Katika makabila ya mashariki ya kati wana miungu yao mikuu ambayo ni; jua, mwezi na nyota kati ya miungu yote, katika miungu hii, Nimrod kuishi kwenye jua, Shemiramis kuishi kwenye Mwezi na motto(Tammuz) kuishi kwenye Nyota 2wafalme23:5. Mambo hayo waisrael walirithi kutoka Babeli, na kuyafanya, warumi pia wameyarith na kuyazingatia kwa kuyarekebisha. Lengo la shetani kufanya mfano huu wa Utatu mtakatifu; yaani wakaufananisha utatu mtakatifu wa mbinguni na miungu yao kama ifuatavyo;

v  MUNGU BABA = mungu jua = Nimrod.

v  MUNGU MWANA = mungu mwezi =Shemiramis.

v  MUNGU ROHO MTAKATIFU = mungu nyota = Tammuz.

CHRISTMAS (KRISMAS).

Kuzaliwa kwa Tammuz, tarehe 24 kuamkia 25 mwezi wa 12 kuliambatana na sherehe iliyofanyika kwa kuzaliwa kwa mtoto Tammuz, Yeremia 7:17- Leo imegeuzwa kuwa ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa YESU Kristo Mwana wa MUNGU jambo ambalo siyo sahihi. Kilicho badilika hapa ni badala ya kutumia jina la Tammuz wamebandika jina la YESU huku wakiendelea na matendo yao maovu hasa katika siku hiyo.

KUFUNGULIWA WAFUNGWA +KUZALIWA KWA TAMUZI =KUZALIWA KWA YESU?

Katika tarehe 25/12 ilikuwa siku ya kusherekea  kuzaliwa kwa Tammuz. Kwa leo wanasherekea  kuzaliwa kwa Yesu ambapo  si kweli, ni mpango wa kuendeleza utukufu wa miungu ile ya zamani. Sikukuu nyingi na sherehe nyingi za kimataifa katika nchi za mashariki huwa zinafanywa kwa kufuata siku maalum zinazotumika katika kuheshimu miungu yao. Kwa mfano 25/12 kila mwaka hutumika kwa kuwaachia  baadhi ya wafungwa kuwa huru, na tangu zamani hata katika taifa la Mungu. Chukulia Tanzania kwa mfano, kila mwisho wa  mwaka Rais anatoa msamaha kwa baaadhi ya wafungwa, ni utamaduni uliorithiwa  tangu huko zamani lakini pia kusherekea kuzaliwa kwa mtoto Tammuz ,ambapo leo anasingiziwa Yesu.

MAAJABU YA SIKU ZA SIKUKUU

Katika siku hizi zote kristmas, pasaka kuna mambo makubwa yanayotendeka siku hiyo,  hata kushangza viongozi  wanchi mbalimbali. Hata wakuu wa dini hubaki kushangaa, ijapo wenyewe ndio  viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali yanayohusika kusimamia, kutetea na  kushawishi kushiriki katika sikukuu hizo. Sikukuu  ya Pasaka, Kristimasi na Ramadhani na Siku ya Wapendanao. Badala ya kuabudu huyo Mungu wa mbinguni siku hizo zimekuwa zikitumika kuongeza maambukizi ya  magonjwa ya  zinaa ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI, kwani watu wengi siku hiyo huzini bila huruma, watu wanaosherekea kwa kuzini na wanawake na wanaume. Ndoa nyingi huwa kwenye  mgogoro.

            Siku hiyo watu hunywa pombe  na kulewa ovyo ovyo, wakiyatoa  matusi mengi na mazito toka  midomoni mwao, ugonvi, kubomoa nyumba na vibanda  vya watu, kupanga mawe njiani, kuchoma Tairi za magari barabarani, watu kuendesha magari ovyo na kwa fujo wakisababisha ajali nyingi na hata za makusudi. Watu wanalewa mpaka wanalala uchi mitaani, “kama unataka kuona uchi wa mkwe wako tegea siku hiyo ya kusherekea akilewa hatajitambua, atajikojolea ovyo, kulala uchi basi nawewe katika kumsaidia ili asiaibike zaidi utakuwa umemuona” . Askari katika dunia nzima hawapumziki nao waifurahie hiyo sherehe bali hukaa chonjo wakipambana na wahalifu wanaozidi na kuongezeka siku hiyo. Siku hizo ni siku za ANASA, Wanyama na ndege wanakuwa na maombolezo makuu kwani si Mbuzi, Ng`ombe, Kuku na wengineo wanaoliwa, huchinjwa bila huruma eti  kwa kuwa Mwanadamu anasherekea.

 MAADIKO MATAKATIFU YANASEMA NINI KUHUSU SIKUKUU HIZI:

Mungu hapendezwi na sikukuu hizi hata kidogo, kwani kama zingekuwa na utukufu ndani yake yasingefanyika machafuko na maovu haya yote. Mungu atakomesha furaha zao na sikukuu zao,(Hosea 2:11, Isaya 24:7-10, Amosi 5:5). Mungu hapendezwi na sikukuu hizi kwani ni kufuru kwake na hakuna fungu lolote katika biblia  linalosema kuwa Yesu alizaliwa tarehe ngapi, na wala katika siku za sikukuu hizi, tuliyofunuliwa na mungu ni yetu na watoto wetu, tusiyofunuliwa hayo ni ya Mungu mwenyewe( tutayafahamu tukifika mbinguni, tutamuuliza Baba habari za mambo hayo tusiyoyajua).

Utaratibu wa sikukuu hizi ni mpango wa shetani kuendelea kuabudiwa na kuabudu miungu kwa kujua au kutojua kwa kutumia pazia lenye jina jingine ili kificha ukweli lakini kiini cha maovu na kufuru kwa Mungu Baba zikiwa zinaendelea kwa kasi siku hizo.

MAMBO UFANYAYO KUSHIRIKI SIKUKUU HIZO BILA KUJUA AU KWA KUJUA.

1)      Kutuma ujumbe kwa simu, kadi na barua au zawadi maalum ya kumpongeza au kumtakia sikukuu njema. Hii inamaana unakubaliana naye juu ya hicho anachotaka kukifanya nawe unamuunga mkono na kumtia moyo asonge mbele.

2)      Kuingia gharama ya kununua mavazi ya kuvaa siku hiyo ya sikukuu. Kama huna mpango wa kusherekea, kwanini unataka ufanane na wenye mtazamo huo wa kuonekana wapya kwa hadhi ya siku hiyo?

3)      Kutumia siku hiyo kuma siku yako ya kutalii na kutemelea sehemu mbalimbali ambazo ni rahisi kukuondoa katika mtazamo wa kiroho.

4)      Kuhudhuria mialiko mbalimbali uliyoalikwa kwa siku hiyo.

                                   MAJINA TOFAUTI YA TAMUZI

            Maana ya jina Tamuzi ni mungu mwili kama tulivyokwishaona, lilikuwa ni jina la kikabila. Lakini hatahivy  Tamuzi alijulikana kwa majina mbalimbali katika sehemu tofauti tofauti.

                               I.            Kisumeri maana ya jina lake ni DUMUZI (mungu wa mavuno na mazao).

                            II.            Kikaanani alijulikana kama BAALI.

                         III.             Kiefeso lilimaanisha ARTEMI.

                         IV.             Asia, lilimaanisha ASHTORETH.

                            V.            Kilatini lilimaanisha ISHTAR.

                         VI.            Kiingereza lilijulikana kama EASTER na

                      VII.            Kiswhahili lilimaaanisha  PASAKA.

MTIRIRIKO WA DOLA ZILIZOMWABUDU TAMMUZ

Tammuz aliabudiwa katika dola zifuatazo:

A.    Dola ya Babeli mwaka 605 B.C hadi 538 B.C.

B.     Waamedi mwaka 538 B.C hadi 331B.C .

C.     Wayunani mwaka 331 B.C hadi 168 B.C   na

D.    Warumi mwaka 168 hadi 478 A.D

N.B; Tammuz aliendelea kuabudiwa kwa namna ambayo ilianzishwa na mfalme wa Rumi ya  kipagani `Constatino mwaka wa 312  A.D` kama ifuatavyo;

1)      Aliidhinisha ibada ya maadhimishonya siku ya jua, Sunday (Jumapili) siku ya kuabudu jua badala ya Sabato (Sturday) siku ya BWANA ambayo ni siku ya saba ya juma (Alibadili sabato ya jumamosi).

2)      Mfalme Constantine pia aliadhimisha siku ya tarehe 25/12 kuwa siku maalumu kwa kuzaliwa Mtoto Yesu, kwa ukweli Mtoto Tammuz alizaliwa tarehe 25 December na kuzaliwa kwake kunaadhimishwa na Ukristo wa leo kama kuzaliwa kwa Yesu. Tarehe 25 ya mwezi wa 12 ilisherehekewa kumkumbuka Mtoto Tammuz katika dola ya Babeli, katika siku hii wafungwa waliofungwa gerezani walifunguliwa na kuwekwa huru. Soma Yeremia 52:31-34.

3)      Sikukuu ya EASTER ambayo inafanyika mwishoni mwa mwezi wa Tatu (March) au mwanzoni mwa mwezi wa Nne (April) ni idhinisho la Tatu lililosimikwa na Mfalme Constantine. Wakristo wanadai kumba ni ibada ya kukumbuka kufa kwa Bwana Yesu. Historia ikowazi katika jambo hili kwamba ni katika kipindi hiki cha EASTER ambapo wapagani walikuwa wanaomboleza kwa kufa kwa Mtoto Tammuz aliyezaliwa tarehe 25 December na kuaminiwa kupatwa na mauti mnamo mwishoni mwa mwezi wa tatu au mwanzoni mwa mwezi wan ne. kwa sasa ni ukumbusho wa kifo cha Yesu na sio Tammuz.(Oxford Dictionary-Constantine History).

4)      Vilevile katika karne ya nne Mfalme Constantine aliadhimisha ibada ya kumuabudu Mama yake Yesu (Bikra Maria) ambaye kwa sura zijazo tutaona jinsi ambavyo Malkia Shemiramis au mke wa Nimrodi aliyepewa jina la Mariamu Mama yake Yesu ili kuingiza upagani katika Ukristo.

MWISHO.

Miongoni mwa sikukuu zilizotajwa hapo juu (krismas,pasaka,ramadhani na siku ya wapendanao), Hakuna hata moja inatoungwa mkono na MAANDIKO MATAKATIFU endapo mtu ataamuwa kushiriki kwa namna yeyote ile ni kwa ukaidi wake mwenyewe. Mambo hayo hayaungwi mkono na maandiko matakatifu wala vitabu vya ROHO YA UNABII. Mambo yanayotendeka ni makufuru kwa Mungu wa Mbinguni.

Somo hili ni sehemu ya kwanza, sehemu ya pili itahusu;

(i)                 Mwanzo wa Ibada ya Mama na Mtoto.

(ii)               Mwanzo wa Ibada yenye matumizi ya Rozali(shanga).

(iii)             Mwanzo wa siku ya wapendanao.

(iv)             Mwanzo wa sikukuu ya Ramadhani.

(v)               Father Santa Clause ni nani?

Bila shaka sasa kila mmoja wetu amegundua ukweli kwamba krismasi ni sherehe ya kipagani  na kwa hivyo anawajibu wa kubadilisha mtazamo wake na kujikita katika maandiko  ili kuendelea kuujua ukweli na kuepuka  kudanganywa .

OGOPA!
#Amkeni Amkeni Wakristu! 

1 comment:

  1. Umetudanganya bhna ww🤣🤣🤣 hyo ya TAMMUZ ni easter
    wazungu wapuuzi saana wanaita pasaka ni esster

    ReplyDelete