Manchester United wameamka, Maguire 🔥
KWANZA ALAMA 3 ...!
✍🏻Manchester United walifanya vitu vingi sana kwa usahihi na mpango wa kocha ulifanikiwa shida ilikuwa kufunga magoli mengi na ndio maana hata goal difference ya United inaelezea
✍🏻Mpango ulikuwa :-
1: Tanua ile back 5 ya Luton kwa Garnacho na Rashy kuwa pembeni zaidi ya uwanja ili ....
2: Kutengeneza space katikati ya wingbacks na outside CBs wa Luton kuishambulia
3: Kuwa na idadi kubwa ya wachezaji pembeni ya uwanja dhidi ya wingbacks wao ( Garnacho + Reguilon Vs Kabore na Rashy + Dalot Vs Alfie ) ili kuwa na mchezaji mmoja zaidi ( create overloads )
4: Kulazimisha Luton kupoteza mpira haraka mara tu baada ya kuupata ( forced turnovers )
5:Kilichowakwamisha United kutofunga magoli mengi ni umaliziaji wao tu leo ... ulikuwa mbovu
✍🏻Luton mpango wao ulikuwa mmoja tu , kuhakikisha wanazuia kwa idadi kubwa ya wachezaji , kufunga njia za katikati ya uwanja na kusubiria
1: Counter attacks
2: Mipira iliyokufa tu .
NOTE
1: Maguire tangu amerejea kikosini anacheza vizuri
2: Umaliziajia kwa United ni shida kubwa sana msimu huu mpaka sasa
3: Chong sijui kwanini alianzia bench , maana alivyoingia aliwapa tabu sana United hasa nyuma ya kiungo chao
4: Hojlund akae chini amalize tofauti zake na EPL , nafasi zile zile anapata UCL anaweka kambani lakini EPL anakosa . Mechi 9 hana goli wala assist .
5: Wanatamani kusema Luton wepesi lakini wakikumbuka walipata sare inabidi wasonye tu 😀😀😀
FT: Man United 1-0 Luton
Post a Comment