𝐌𝐀𝐌𝐁𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐇𝐀𝐍𝐆𝐀𝐙𝐀 𝐀𝐋𝐈𝐘𝐎𝐘𝐀𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐉𝐈𝐉𝐈 𝐊𝐖𝐀𝐎 𝐘𝐀𝐈𝐒𝐇𝐓𝐔𝐀 𝐃𝐔𝐍𝐈𝐀
➪Sadio Mane ni mmoja ya wachezaji wachache wanojali familia zao, Mane sio mzaliwa wa jiji kuu la Senegal Dakar wala Kaolack ambayo ni majiji makubwa katika taifa hilo bali Sadio Mane ni mzaliwa wa mbambaly anabadilisha kijiji chake kuwa mji.
➪Mane katika kijiji chao ambapo inakadiriwa wanaishi takribani watu 2,000 alijenga hospitali yenye thamani ya £455,000 sawa na Tsh 1,114,993,679/= ambayo itahudumia vijiji 34.
➪Hii inatokana na tukio linalomsumbua sana maishani mwake ambapo baba yake Sadio Mane alifariki dunia wakati Mane alipokuwa na umri wa miaka 7 kwa sababu hapakuwa na hospitali kijijini kwao hivyo akaamua kujenga hospitali yenye kila huduma, Mane na dada yake inaelezwa walizaliwa nyumbani kwa sababu hakukuwa na hospitali. Alijenga hospitali ya kwanza katika kijiji hicho mnamo mwaka 2019.
➪Mane amejenga Shule yenye thamani ya €250,000 ambazo ni sawa na Tsh 612,633,890/= ambayo wanafunzi wanasoma bure, katika kijiji chake cha Bambaly ambacho kipo umbali wa zaidi ya Kilometa 400 kutoka jiji kuu Dakar.
➪Inaelezwa kuwa Mane anaipa kila familia €70 sawa na Tsh 171,537/= kila mwezi mbali na hilo Mane amesaidia upatikanaji wa Inernat kwa kiwango cha 4G kwa ajili ya watu wake wa Bambaly.
➪Mengi zaidi Mane amejenga kituo cha mafuta na posta pia alitoa kompyuta mpakato zenye thamani ya $400 ambazo bei yake moja sawa na 932,800/= kila moja kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi Shule za Upili huko Bambali.
➪Kubwa zaidi Mane anatoa nguo za michezo bure kwa watoto katika kijiji. Kuonyesha namna anavyowatahamini watu wake na kuwapenda kila akipata likizo huenda nyumbani kwao Bambaly na kucheza mpira wa mtaani Sodo pamoja na vijana wa mtaani licha ya kujenga sehemu nzuri za kuchezea mpira.
➪Mane ni mchezaji w atofauti sana, kama mnakumbuka alikuwa anatumia simu iliyopasuka kioo mpaka mchezaji mwenzake wa liverpool Lovren akaona haifai ikabidi akamnunulie iPhone 12 mpya ila Mane alipoulizwa alijibu kuwa simu mpya, Magari ya kifahari, Ndege za kifahari na vito vya thamani kwake havina thamani na haviwezi kuwa msaada kwa watu wake.
➪Inaelezwa na watu wa karibu kuwa Mane yupo radhi kulala chini ila amuone raia wake kutoka Bambaly anaishi maisha ya furaha.
Post a Comment