𝐒𝐀𝐋𝐀𝐇 𝐀𝐆𝐀𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐋𝐈𝐎𝐍𝐈 𝐍𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐀 𝐅𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐖𝐀𝐎


 ➪Mshambuliji wa Kimataifa wa Liverpoo na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah amekuwa mfano mzuri wa akuigwa kwa namna anavyojaribu kubadilisha mandhari ya kijini alipozaliwa huko nchini Misri.


➪Kijiji hicho kinachojulikana kwa jina la Nagrig nchini Misri kipo umbali wa kilometa 124.2 kutoka Kaskazini mwa jiji la Cairo.


➪Ikumbukwe Salah sio mzaliwa wa Cairo wala majiji makubwa misri kama Cairo, Alexandria, Salah inaelezwa kuwa katika kijiji chao amejenga hospitali, shule, kituo cha vijana cha michezo na kitengo cha magari ya wagonjwa kwa watu wake katika kijiji chake.


➪Mbali na hilo Salah amejenga kituo cha kuratibu maji safi kinachoelezwa kugharimu $450,000 sawa na T sh 1,049,400,000/= ili kutoa maji ya kunywa kwa watu wake.


Kubwa zaidi Salah anatoa £3,500 sawa na Tsh 8,162,000 kwa familia maskini kila mwezi katika kijiji chake.

No comments