𝐓𝐄𝐓𝐄𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐒𝐎𝐊𝐀 𝐔𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐉𝐔𝐌𝐀𝐓𝐀𝐍𝐎 22/06/2022


 ➪Klabu ya Inter Milan ya Italia imekubali dili la kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Chelsea.


➪The Blues walimsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Inter kwa pauni milioni 97.5 mnamo Agosti 2021, lakini atarejea katika kikosi hicho cha Serie A ambacho kilikuwa na matatizo msimu uliopita.


➪Ada ya mkopo kwa Lukaku ni takriban euro 8m (£6.9m).


➪Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alifunga mabao 15 katika michuano yote msimu uliopita akiwa na Chelsea, na mabao manane katika mechi 26 za Premier League.(BBC Sports)


➪Mshambulizi wa Poland Robert Lewandowski bado anataka kuondoka Bayern Munich, licha ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Ujerumani Hasan Salihamidzic kusafiri kukutana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ana kwa ana kujaribu kubadilisha mawazo yake.  (Sky Germany)


➪Real Madrid wameongeza nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling katika wiki za hivi karibuni, huku Barcelona na Chelsea wakifuatilia maendeleo kuhusu mustakabali usio na uhakika wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika klabu ya Manchester City. (Mirror) 


➪Real Madrid, Bayern Munich na Paris St-Germain wako tayari kuchuana na Newcastle United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 20, kutoka Reims. . (L'Equipe - in French) 


➪Ekitike, hata hivyo, yuko tayari kurejea kutoka likizoni mapema kukamilisha uhamisho wa £26.5m kwenda Newcastle. (Chronicle)


➪Barcelona wanataka kumsajili beki wa Ufaransa Jules Kounde, lakini hawataki kulipa euro milioni 60 za Sevilla (£51.5m) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Marca) 


➪Brentford haijakata tamaa ya kumsajili mchezaji wa Denmark Christian Eriksen, ambaye alijiunga nao kwa mkopo mwezi Januari kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita. Manchester United pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30(90 Min)


➪Arsenal na Newcastle wanamtaka kiungo wa kati wa Uhispania Fabian Ruiz, 26, ambaye mkataba wake na Napoli utakamilika 2023.  (Corriere dello Sport, via Mail)


➪Chelsea wanavutiwa na beki wa pembeni wa Lens, 29, Jonathan Clauss. (Goal)


➪Tottenham wanatazamia kufanya mazungumzo zaidi ya kumsajili beki wa kulia wa timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21, Djed Spence kutoka Middlesbrough. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikaa msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Nottingham Forest na kuwasaidia kupandishwa daraja hadi Ligi ya Premia. (Sky Sports) 


➪Borussia Dortmund, ambayo ilimuuza mshambuliaji wa Norway Erling Haaland mwenye umri wa miaka 21 kwa Manchester City, inatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast Sebastien Haller kutoka Ajax kwa euro 36m (£31m).  (ESPN)


➪Wolves wanatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Brazil Gabriel Barbosa, 25, kutoka Flamengo na kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, 21, kutoka River Plate. . (90 Min)


➪Rangers wanaweza kumuuza mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos ikiwa hawatakubali mkataba mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika msimu wa joto 2023. (90 Min) 


➪Manchester United wanatarajia fowadi wa Ufaransa Anthony Martial kuwa katika klabu hiyo msimu ujao kwa sababu ya kutovutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Manchester Evening News)


➪Manchester United wanamfikiria mlinda mlango wa Watford na Austria Daniel Bachmann kama msaidizi wa mchezaji wa kimataifa wa Uhispania David de Gea, 31, huku Mwingereza Dean Henderson, 25, akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford na kujiunga na Nottingham Forest. mkopo (Goal)

No comments