Je Brazil watabeba Kombe la Dunia mwaka huu 2022 Qatar?
Brazil tayari wamekata tiketi ya kushiriki kombe la Dunia 2022 huko Qatar na jana wamempa Chile mabao 4 ktk kuhakikisha wanamaliza nafasi ya kwanza mbele ya Argentina kwa heshima.
lakini bado kazi kubwa kwao ni kutafuta kunyanyua kombe la Dunia ambalo mara ya mwisho kwao, CAFU ndiye aliyenyanyua kama nahodha mwaka 2002 baada ya ushindi wa fainali vs Ujerumani.
.
Huyu jamaa alivaa usinga akiwaongoza Ronaldo de Lima, Rivaldo, Gaucho, Leonardo, Dida, Marcos, Kaka na wengine.
.
Haya hapa ndiyo yaliyo nyuma yake mpaka kuona akivaa usinga mbele ya nyota hao wakubwa wa nchi kubwa ya soka kama Brazil:
.
1. Ndiye mchezaji pekee Duniani kucheza fainali TATU mfululizo za kombe la Dunia (1994, 98 & 2002) akishinda mbili kati ya hizo (1994&2002)
.
2. CAFU ni mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi akiwa na uzi wa timu ya taifa ya Brazil ( mechi 12 )
.
3. Wakati akizitumikia klabu za Italia, uwezo wake wa kupanda na kushuka kwa kasi ulifanya mashabiki kumpa jina la utani Pendolino akifananishwa na treni ya mwendokasi ya umeme nchini humo.
- Hilo pia liliwahi kufanya Sir Alex Ferguson kusema " CAFU ana mioyo miwili ".
.
4. Jamaa ametwaa tuzo kibao ikiwemo:
- mchezaji bora wa Amerika Kusini 1994
- kikosi bora cha Ballon D Or Cha muda wote (Ballon D Or Dream Team).
- kikosi bora cha karne ya 21
.
5. pamoja na hayo mafanikio yote huwezi amini jamaa wakati kijana alikataliwa na timu 5 za vijana Brazil ( Corinthians, Santos, Palmeiras, Atletico Mineiro na Portuguesa ) wakiamini hakuwa na uwezo kabla ya kuchukuliwa na timu ya nyumbani Sao Paulo na ndio mwanzo wa rekodi na historia kubwa kwake.
.
NB : maandishi kwenye jezi yake hapo pichani ni " 100% Jadim Irene " ni eneo alilokulia huku anasema alifanya hivyo kuonyesha vijana kuwa inawezekana ukatokea ktk mitaa isiyo na utajiri na bado ukawa bingwa, mchezaji mashuhuri na mtu mwema kwa wengine na pia aliitoa tuzo hiyo kwa mke wake Regina.
Post a Comment