Morrison Aomba Msamaha Simba SC
𝐁𝐄𝐑𝐍𝐀𝐑𝐃 𝐌𝐎𝐑𝐑𝐈𝐒𝐎𝐍 𝐀𝐎𝐌𝐁𝐀 𝐑𝐀𝐃𝐇𝐈
➪Imeelezwa kuwa Staa wa Simba, Bernard Morrison 🇬🇭 ametuma ujumbe kwenye kundi la WhatsApp la wachezaji wa timu hiyo na kufowadi vilevile kwa viongozi akiomba radhi kwa kilichotokea.
➪"Naomba radhi kwa wachezaji, kocha, meneja, kapteni na wachezaji wazoefu na kila mmoja aliyepo humu. Naomba radhi sana kwa yale yote yanayoendelea na yaliyotokea kwani naamini nimefanya jambo la kutowaheshimu kila mmoja wenu, najua nimeikosea klabu na sikulenga kufanya hivyo,
➪"Lakini kwa jambo lililotokea haina maana kwangu kujielezea binafsi naomba msamaha kutoka kwenu wote, naomba msamaha kwenu, John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Joash Onyango, Clatous Chama siwezi kuwataja Wote hapa, ila naomba kwenu wote mnisaidie kuomba radhi kwa kocha na Bodi ya Wakurugenzi.
➪“Nina imani baada ya hapo nakwenda kufanya vitu vilivyokuwa bora natamani amani iwepo pamoja na upendokwa mara nyingine tena. Naomba mnisamehe jamani. Nimekosa.
.
vipi WANASIMBA mmesamehe __!!👀
Post a Comment