AMKA NA BWANA LEO 10/02/2022

KESHA LA ASUBUHI 

ALHAMISI, FEBRUARI 10 2022

KRISTO, MFANO WA UTII WA KWELI

Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. Warumi 6:16.

📚 Adamu hakukoma kuhesabu matokeo ya kutokutii kwake.... Pamoja na ufahamu wa baadaye tuliobahatika kuwa nao, tunaweza kuona kile inachomaanisha kutokutii amri za Mungu. Adamu alishindwa na majaribu, tunapokuwa na suala hili la dhambi na madhara yake yakiwekwa dhahiri mbele yetu, tunaweza kusoma kutoka kwa visababishi hadi katika athari na kuona ukubwa wa kitendo sio kile kinachounda dhambi; bali kukosa utii kwa mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa; ambako ni kumkana Mungu kisirisiri, kuzikataa sheria za serikali Yake.

📚 Furaha ya wanaume kwa wanawake iko katika utii wao kwa sheria ya Mungu. Katika utii wao kwa sheria ya Mungu wamezungukwa kama vile ua na kutunzwa kutoka katika uovu. Hawawezi kuwa na furaha na kukwepa mahitaji maalumu ya Mungu, na kuweka viwango vyao wenyewe, ambavyo wanaamua kuwa wanaweza kuwa salama kuvifuata. Hapo basi kutakuwa na viwango mbalimbali ili kupelekana na akili tofauti, na serikali [itakuwa] imetwaliwa kutoka katika mikono ya Bwana na wanadamu [wange] shika hatamu ya serikali. Sheria ya ubinafsi inasimamishwa, mapenzi ya wanadamu yamefanywa ya juu, na wakati mapenzi ya juu na matakatifu ya Mungu yanawasilishwa ili kutiiwa, kuheshimiwa na kuadhimishwa mapenzi ya mwanadamu yanataka njia yake yenyewe kufanya mambo yake yenyewe, na kunakuwa na pambano baina ya wakala wa wanadamu na Mungu.

📚 Anguko la wazazi wetu wa awali lilivunja mnyororo wa thamani wa utii kamili wa mapenzi ya mwanadamu kwa Mungu. Utii haujaonekana tena kuwa wa lazima kabisa. Mawakala wa kibinadamu wanafuata fikra zao wenyewe, ambayo Bwana alisema juu ya wenyeji wa ulimwengu wa zamani kuwa walikuwa waovu hivyo na tena bila kukoma. Bwana Yesu anatangaza, "Nimezishika amri za Baba Yangu." Ki vipi? Kama mwanadamu. Tazama, nimekuja nifanye Mapenzi Yako, Ee Mungu. Mbele za shutuma za Wayahudi alisimama katika usafi, uadilifu, tabia Yake takatifu, na kuwapa changamoto, "Ni nani miongoni mwenu

🔘 Mwana pekee wa Mungu asiye na mwisho amesema, kwa maneno anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?" Yake, kwa mfano wa utendaji Wake, ametuachia mfano dhahiri ambao sharti tuufuatishe. Kwa maneno Yake ametufundisha kumtii Mungu, na kwa utendaji Wake ametuonesha jinsi tuwezavyo kumtii Mungu.
MUNGU AKUBARIKI SANA

*LESONI LEO.*

Alhamisi, 10/02/2022.

*YESU, NANGA YA ROHO.*

Usomaji wa Biblia: Mwanzo 28.

Paulo anahitimisha onyo lake dhidi ya uasi na faraja kwa upendo na imani kwa maelezo mazuri, yanayopanda juu ya uhakikisho katika Kristo.

Soma Waebrania 6:17-20. Mungu alituthibishiaje ahadi zake?

Mungu alithibitisha ahadi zake kwa ajili yetu kwa njia kadha wa kadha. Kwanza, Mungu aliithibitisha ahadi yake kwa kiapo (Ebr. 6:17). Kulingana na Maandiko, viapo vya Mungu kwa Ibrahimu na Daudi vilikuwa msingi wa mwisho wa ujasiri katika fadhila za Mungu za kudumu kwa Israeli. Wakati Musa alipotafuta kupata msamaha wa Mungu kwa ajili ya Israeli baada ya uasi kwa ndama wa dhahabu, alirejelea kiapo cha Mungu kwa Ibrahimu (tazama Kut. 32:11-14, Mwa. 22:16-18). Nguvu iliyodokezwa ya ombi lake ilikuwa kwamba kiapo cha Mungu kilikuwa kisichobadilika (Rum. 9:4; Rum. 11:28, 29).

Hali kadhalika, wakati mtunga Zaburi alipowaombea Israeli mbele za Mungu, alikidai kiapo cha Mungu kwa Daudi. Mungu alisema: “ ‘Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo, Wazao wake watadumu milele, Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu. Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.’ ” (Zab. 89:34-37). Kulingana na Agano Jipya, viapo vyote vilitimizwa katika Yesu, mzao wa Ibrahimu, aliyepaa na kukalia kiti cha Daudi (Gal. 3:13-16; Lk. 1:31-33, 54, 55).

Pili, Mungu amezithibitisha ahadi zake kwetu kwa kumketisha Yesu mkono wake wa kuume. Kupaa kwa Yesu mbinguni kuna kusudi la kuthibitisha ahadi iliyotolewa kwa waumini kwa sababu Yesu alipaa mbinguni kama “mtangulizi kwa niaba yetu” (Ebr. 6:20, msisitizo wa mtunzi).

Hivyo, kupaa kwa Yesu kunatufunulia uhakika wa wokovu wa Mungu kwetu. Mungu alimwongoza Yesu katika utukufu kupitia mateso ya “mauti kwa ajili ya kila mtu,” ili aweze kuwaleta “wana wengi waufikilie utukufu” (Ebr. 2:9, 10). Uwepo wa Yesu mbele za Baba ni “nanga ya roho” (Ebr. 6:19), iliyosimikwa katika kiti cha enzi cha Mungu. Heshima ya utawala wa Mungu imeendelezwa katika utimizwaji wa ahadi yake kwetu kupitia kwa Yesu. Uthibitisho gani zaidi tunahitaji?

Unahisi nini unapofikiri kwamba Mungu amekuapia? Kwa nini wazo hilo pekee linapaswa kusaidia kukupa uhakika wa wokovu, hata unapohisi kutokustahili?

No comments