UNA NINI MKONONI MWAKO?

UNA NINI MKONONI MWAKO?
(Makala ya 7 Kati ya 100 mwaka huu 2022)

Binafsi naamini kila mtu anacho kitu fulani Cha maana Sana mkononi mwake. 

Haijalishi inaweza kuwa kidogo kiasi gani kulinganisha na walivyo navyo wengine. Lkn ili mradi Ni Cha kwako Basi tambua kuwa kina maana kubwa 

Muhimu Ni kujifunza kuheshimu kwanza ulichonacho huku ukiwa na imini kwamba kupitia hiko kidogo ulicho nacho unaweza kufanya mambo makubwa mno.

Mkononi mwako unaweza kuwa na pesa kidogo lkn unatamani kufanya Mambo makubwa, hiyo isikuvunje moyo. Anza kuchukua hatua kwa kile kidogo ulichonacho kwasababu pesa haijawahi kutosha.

Mkononi mwako unaweza kuwa na kipaji fulani na unatamani kufika mbali, usife moyo na kuacha kukionyesha kipaji chako mbele za watu kwasababu tu hakuna anayekusifia au kukushika mkono.

Kila kilicho kikubwa bila Shaka kilianza kuwa kidogo. 

Waswahili husema mbuyu ulianza kma mchicha. Msemo ambao humaanisha kuwa, kila kitu kinakwenda kwa hatua. Huwezi kuwa mzee Kama hujawahi kuwa mtoto au kijana.

Katikati ya mchakato huo wa kuvuka hatua moja kwenda hatua nyingine zipo changamoto chungu nzima.

Hicho ndicho hutokea hata kwetu pia tunapokuwa tunataka kuvikuza vile vidogo tulivyonavyo mkononi ili viwe vikubwa. Ni lazima kutakuwa na changamoto.

Lakini pamoja na changamoto hizo, uvumilivu, Uthubutu, kutokukata tamaa, Nia, juhudi na nidhamu Ni Mambo ya msingi katika mchakato wa kuvikuza vile vidogo tulivyonavyo mikononi ili viwe vikubwa.

   Kumbuka Usisahau; Usipende kutamani vikubwa walivyonavyo wengine pasipo kujua walipitia ugumu gani mpaka kuwa navyo. Tembea kwa miguu yako ili uache nyayo zako.✋✋✋
Writer; Jofrey Mwanambesi
Page Facebook; Ghala la kumbukumbu
📞📞 0759606160/0623758540

No comments