SIKU YA CHAKULA DUNIANI KUFANYIKA MOSHI, KILIMANJARO
Mhe. Prof Adolf Mkenda amesema kuwa, wakati wa maadhimisho hayo shughuli zifuatazo zitafanyika ili kufikia malengo na madhumuni yaliyoorodheshwa hapo juu;-
1. Maonesho ya kazi mbalimbali zinazolenga kuongeza uzalishaji, tija na upatikanaji wa chakula na usindikaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
2. Kutoa elimu juu ya kuandaa vyakula mbalimbali, lishe bora, uhifadhi na usindikaji wa mazao ya chakula, mifugo na uvuvi katika ngazi ya kaya na jamii.
3. Kutoa elimu ya matumizi ya mbegu za asili na mchango katika Usalama na Uhakika wa chakula na maendeleo ya Taifa.
4. Kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa na ufahamu kuanzisha bustani, ufugaji wa wanyama wadogo wadogo, umuhimu wa lishe bora na ujuzi wa kuandaa mlo kamili.
5. Kuhamasisha uzalishaji na matumizi ya vyakula vya asili katika ngazi ya kaya na jamii.
Post a Comment