GEUWASA KUZINGATIA WELEDI KATIKA UTOAJI HUDUMA

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Geita,(GEUWASA) imewahakikishia wateja wake ambao wamekuwa wakipatiwa huduma ya maji safi na maji taka kuendelea kutoa huduma hiyo kwa kuzingatia weledi na kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza kwenye baadhi ya maeneo ambayo huduma za maji zinatolewa.

Hayo yamesemwa mapema leo na mkurugenzi mtendaji wa GEUWASA ,Mhandisi Frank Changawa wakati hafla fupi ya kutambua mchango wa wateja ambao wamekuwa wakipatiwa huduma ya maji mjini Geita.

“GEUWASA bila nyie wateja wetu hatuwezi kufanya shughuli zetu tunatambua umuhimu wenu na tunawahaidi kuendelea kuboresha utoaji wa huduma zetu ili tuendane na sera yetu ya maji yetu uhai wetu kwa sababu tunajua maji ni uhai na ndio maana tumeendelea kuboresha miundombinu ya maji kwa kuongeza upanuzi wa maeneo ambayo hayajafikiwa na maji kwa wepesi”---- Frank Changawa Mkurugenzi Mtendaji wa GEUWASA.

“Lakini pia bado tunamikakati ya muda mfupi wa kuwachimbia watu visima pamoja na kuweka matenki kwenye maeneo ambayo yanaonesha kuna shida kubwa ya upatikanaji wa maji sanjali na ilo mpango wetu wa muda mrefu bado tunaendelea nao wa kutoa maji ziwa viktoria ili tuweze kusambaza maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hii muhimu”---- Frank Changawa Mkurugenzi mtendaji GEUWASA

No comments